Miongoni mwa harakati zake za kielimu zinazo lenga kwendana na maendeleo ya Dunia katika sekta ya udaktari, na kwa ajili ya kupata uzowefu na kuwajengea uwezo watumishi wake, hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya imeandaa warsha kuhusu athari za unene kwa kushirikiana na shirika la (INGENIOUS) na kuangalia njia za kisasa za kupambana na tatizo hilo, ikiwa ni pamoja na njia ya upasuaji na kupunguza nyama za tumbo.
Warsha hiyo imefanyika ndani ya ukumbi mkuu wa haspitali na kuhudhuriwa na madaktari wabobezi katika sekta hiyo, wanaofanya kazi katika Hospitali ya Alkafeel na kutoka idara ya afya ya mkoa wa Karbala pamoja na mikoa mingine, katika warsha hiyo wamejadili njia za kisasa za upasuaji zinazo tumika kutibu tatizo la unene, hospitali ya rufaa Alkafeel inanafasi kubwa katika swala hili kutokana na kufanya kwake ubasuaji mara kadhaa uliotoa mafanikio.
Daktari wa upasuaji Liith Sharifiy kutoka hospitali ya rufaa Akafeel na daktari wa upasuaji Hassan Wahabi kutoka Lebanon wametoa ufafanuzi kuhusu njia za kisasa zinazo tumika katika upasuaji, na wakaonyesha video na kutembelea chumba cha upasuaji kwa ajili ya kuangalia vifaa tiba vinavyo tumika katika upasuaji huo.
Shirika la (INGENIOUS) limeonyesha vifaa tiba vya kisasa zaidi vinavyo weza kusaidia kuondoa tatizo hili.
Katika ujumbe rasmi uliowasilishwa kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel Dokta Liith Sharifiy amebainisha kua: “Hospitali ya rufaa Alkafeel huu ni mwaka wa nne mfululizo imekua ikifanya warsha za mambo ya tiba, leo warsha yetu inamambo mengi ya kufurahisha ukizingatia kua Iraq ni taifa pekee katika mataifa ya kiarabu ambalo linauwezo wa kufanya ubasuaji wa kupunguza unene, na jambo lingine sisi tutaanzisha jumuiya ya kiiraq itakayohusika na swala la unene”.
Kiongozi mkuu wa shirika linalo husika na kutoa huduma za kitabibu na mwakilishi wa shirika la (INGENIOUS) hapa Iraq Ustadh Ammaar Zuhair Dabbaagh amesema kua: “Katika warsha hii tunakusudia kuinua kiwango cha utowaji wa huduma za afya na kuboresha upasuaji wa kupunguza unene, pamoja na kuweka mazingira ya kuwasiliana kati ya hospitali kubwa za kimataifa na hospitali za Iraq, ikiwa ni pamoja na huospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ni moja ya hospitali kubwa hapa Iraq”.