Ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s): Usomaji wa Qur’ani watanda na kuhusisha mazuwaru pamoja na kuitafakari…

Maoni katika picha
Jioni tukufu ndani ya mwezi wa Rabiul Awwal umefanyika usomaji wa Qur’ani, ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mazuwaru wameshiriki katika kikao hicho cha usomaji wa Qur’ani sambamba na kufanya tadaburu kwa unyenyekevu, wamekaribishwa wasomaji wa Qur’ani kutoka katika Maahadi ya Qur’ani tukufu mkoani Baabil katika mahfali ya usomaji wa kila wiki, unaosimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na Hussein Haadi msomaji wa tawi la Maahadi katika mji wa Baabil na mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, kisha kikafuata kisomo cha Hassan Dhabhaawi mmoja wa wanafunzi wa semina inayo fanywa na kituo cha mradi wa Qur’ani na msomaji wa mazaru ya Imamu Qassim (a.s), halafu akafuata Muhsin Ramahi kutoka mkoa wa Baabil, na mwisho akasoma Muhammad Ridhwa Salmaan ambaye ni msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya inaendesha miradi mingi ya Qur’ani, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilaawah, nao ni mradi unaolenga kunufaika na vipaji pamoja na uwezo mkubwa wa usomaji wa Qur’ani walionao vijana wa kiiraq na kuutangaza katika ulimwengu wa kiislamu, sambamba na kuendeleza vipaji hivyo ndani ya utaratibu maalum uliowekwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: