Idara ya kujibu maswali ya kisheria inafanya kazi kubwa ya kujibu maswali kutoka kwa mazuwaru…

Maoni katika picha
Miongoni mwa idara zinazo fanya kazi kubwa katika kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya ni idara ya kujibu maswali ya kisheria, inajukumu la kujibu maswali ya watu wanaokuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi, idadi kubwa ya mazuwaru huenda katika idara hii ambayo makao makuu yake yapo ndani ya uwanja wa haram tukufu, huuliza mambo yanayo husu maisha yao na changamoto wanazo kutana nazo.

Tumeongea na rais wa kitengo hiki Shekh Swalahu Karbalai amesema kua: “Kitengo chetu kinamajukumu mengi, miongoni mwa majukumu yake ni kujibu maswali yanayo elekezwa katika kitengo hiki, masayyid na mashekh wanaofanya kazi katika kitengo hiki hujibu maswali hayo, wakipata swali gumu lenye utata wanapiga simu kwenye ofisi za fatwa za Marjaa Dini mkuu kwa ajili ya kupata jawabu la swali hilo”.

Akaongeza kusema kua: “Idara hii inafanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa tisa jioni kila siku, ispokua siku za ziara na matukio maalumu huendelea kujibu maswali na kufafanua mambo ya kisheria hadi usiku, na hukutana na watu katika ofisi zote nne, ambazo ni:

  • a- Ofisi ya baina ya haram mbili.
  • b- Ofisi ya mlango wa Algamiy.
  • c- Ofisi ya maqaamu Swahibu Zamaan (a.f).
  • d- Ofisi ya ndani ya haram upande wa (wanaume)”.

Akabainisha kua: “Pamoja na jukumu hili kitengo hiki pia kinaendesha swala za jamaa kila siku ndani ya uwanja wa haram tukufu, na hushiriki katika makongamano na mahafali yanayo fanyika kila siku ndani na nje ya Ataba tukufu, pamoja na kutoa mawaidha ya kidini na kutoa maelekezo mbalimbali kwa waumini sambamba na kufanya semina za kifiqhi na zinginezo kama vile semina za hija na umra”.

Kumbuka kua kitengo cha Dini ni miongoni mwa vitengo muhimu katika Atabatu Abbasiyya, kina watumishi ambao ni wasomi wakubwa wa hauza (vyuo vya kiislamu), wanaotoa huduma kubwa tena kwa unyenyekevu na heshima kubwa kutokana na utukufu wa mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s). kwa maelezo zaidi kuhusu shughuli zinazo fanywa na kitengo hiki tembelea toghuti ifuatayo: https://alkafeel.net/religious/.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: