Maonyesho ya kazi za kiufundi ni moja ya harakati zinazo fanywa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, lengo kuu la maonyesho haya ni kuenzi utukufu wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), na yanayo fanywa na wapenzi wake wanapokuja kumtembelea na wale wanao wahudumia mazuwaru wake, kitengo kinafanya maonyesho ya picha katika malalo ya Saidi bun Jubeir (r.a) kwenye mji wa Hai, uliopo kusini mwa mkoa wa Waasit umbali wa kilometa (45) takriban, kufuatia kumbukumbu ya kifo chake, maonyesho yanafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ashura ni alama ya kudumu) na yamehusisha picha (50). Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukfu Husseiniyya na Abbasiyya, kimefanya maonyesho ya picha karibu na kaburi la Saidi bun Jubeir (a.s) katika harakati zake, picha hizo zilipigwa wakati wa ziara ya Arubani na matukio mbalimbali yaliyo tokea kwa wahudumu wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya na huduma zilizo tolewa na Ataba mbili tukufu”.
Akaongeza kua: “Washiriki wa maonyesho haya wanatoka katika kitengo cha habari na utamaduni pamoja na wapiga picha wa kitengo chetu, jumla ya mabango yanayo shiriki ni (50) yenye ukubwa wa (60X49sm), zinazo onyesha matukio ya maombolezo ya Imamu Hussein (a.s) pamoja na matembezi ya mamolioni ya watu na huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru, ikiwa ni pamoja na kuonyesha ufundi na umahiri wa kupiga picha katika kipindi za huzuni cha Ashura na Safar”.
Akaendelea kusema kua: “Katika maonyesho haya tumejaribu kuonyesha tukio hilo kwa kutumia picha, na kulifanya kuwa kumbukumbu muhimu kwa vizazi vijavyo, na kutoa picha kwamba Ataba tukufu zinanafasi kubwa kiroho, kiutamaduni na kiitikadi, bali ndio kitovu cha kuwajenga watu kiakili na kimazingira”.
Kumbuka kua maonyesho haya ni sehemu ya mfululizo wa maonyesho ya picha yanayo fanyika ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala katika tukio la furaha au huzuni za watu wa nyumba ya Mtume (a.s) sambamba na harakazi za mazuwaru wanaokuja kutembelea malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).