Mapambo yenye umri zaidi ya karne moja: Mlango wa Qadhi katika sardabu ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), angalia vitu muhimu ndani makumbusho ya Alkafeel…

Maoni katika picha
Makumbusho ya vifaa na nakala kale ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetunza vifaa kale vingi vinavyo endana na utukufu wake, miongoni mwa vifaa hivyo ni mlango wa Qadhi uliokua katika sardabu tukufu upande wa mashariki ya haram, nao ni miongoni mwa turathi muhimu katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na unaumuhimu mkubwa katika makumbusho haya.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha makumbusho Uatadh Swadiq Laazim aliyo uambia mtandao wa kimataifa Alkafeel: “Ni mlango wa fedha uliowekwa nakshi za maua mazuri na kupambwa kwa aya za Qur’ani tukufu, uliondolewa na kuwekwa mahala pake mlango wa dhahabu mwaka (2008m), mlango huo uliwekwa tangu mwanzoni mwa karne ya ishirini”.

Akaongeza kua: “Umefanyiwa marekebisho na wataalamu wa makumbusho kwa ajili ya kuutunza na kuuweka ndani ya makumbusho ya Alkafeel, umeondolewa kutu na kusafishwa kwa kutumia vifaa maalumu, kisha ukawekwa Burlood kwa (%5) na kuhifadhiwa ndani ya makumbusho kwa ajili ya maonyesho, umekua kimbilio kwa kila anayetembelea makumbusho hii”.

Akasema: “Kuna umuhimu mkubwa wa kuonyesha vifaa vilivyo tolewa katika haram tukufu, Atabatu Abbasiyya tukufu inaheshimu sana turathi zilizo tolewa katika haram tukufu, kuanzia vipande vya dhahabu, milango, na vipande vilivyo toka katika minara miwili mitukufu, kwa ajili ya kumjulisha zaairu yaliyo tokea katika mji wa Karbala na katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), ni jukumu la makumbusho kutunza na kuhifadhi vifaa hivi vitukufu vyenye historia kubwa na matukio mengi, pamoja na kua ni ukumbusho mkubwa uliojaa utukufu”.

Fahamu kua makumbusho ya vifaa na nakala kale ni makumbusho ya kwanza kufunguliwa katika levo ya Ataba za Iraq, ilifunguliwa mwaka (2009m) katika maadhimisho ya kuzaliwa bibi Zainabu (a.s), makumbusho hii imesheheni turathi zinye historia ya karne na karne.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: