(Sayyid Ali Husseini Sistani ni mtu mwenye msimamo wa kitaifa na kibinaadamu): hilo ni jina la kitabu kipya kilicho tolewa na kitengo cha habari na utamaduni…

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati za uandishi zinazo fanywa na idara ya masomo na usambazaji chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ni kitabu kipya kilicho pewa jina la: (Sayyid Ali Husseini Sistani ni mtu mwenye msimamo wa kitaifa na kibinaadamu), kimeandikwa na Hassan Ali Jawaadiy mmoja wa watumishi wa idara hiyo, katika kitabu hicho; amenukuu sehemu za khutuba za Marjaa Dini mkuu alizotoa kufuatia matukio mbalimbali yaliyo ikumba Iraq, likiwemo tukio la kuvamiwa na magaidi wa Daesh, na namna khutuma hizo zilivyo zindua watu na kuwafanya wakupali kujitolea kwa ajili ya kunusuri taifa lao na maeneo matukufu, pamoja na msimamo wake wa kulingania kusameheana na kuishi kwa amani bila ubaguzi wala chuki za kikabila na kitabaka.

Mwandishi wa kitabu Hassan Ali Jawaadiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Natija (matokeo) ya kitabu hiki ni kuonyesha namna Marjaa Dini mkuu anavyo jali taifa na wananchi wake, mara nyingi sana amesisitiza juu ya mambo mawili hayo katika khutuba za Ijumaa, amezitaja jamii zote za wachache na tabaka zote za raia, amehimiza uzalendo na kukemea ubaguzi, na wala asipatikane mtu wa kujinufaisha kwa kutumia watu wengine, huo ndio msimamo wake utakao kumbukwa katika historia siku za mbele”.

Akaongeza kua: “Kitabu kimetaja vitu kwa mtiririko, kuanzia kutolewa kwa fatwa tukufu ya kihistoria iliyo leta ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh hadi katika khutuba ya ushindi, na kuonyesha picha ya khutuba za kizalendo kuanzia maneno yanayo tumika na mfumo wa khutuba, kisha akaonyesha namna alivyo toa misaada ya kibinaadamu”.

Kumbuka kua idara ya masomo na usambazaji ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasia inaendelea kutoa vitabu vya kujenga uwelewa kwa vijana wa kiislamu, sambamba na kuzipatia maktaba vitabu vya kisasa vinavyo endana na mtaala wa elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: