Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati kinaendesha mradi wa (Sisi na ulezi wa shule) na chatoa wito kwa wasomi na watafiti kushiriki katika mradi huu…

Maoni katika picha
Kituo cha kiislamu na masomo ya kimkakati ambacho kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa wito kwa watafiti na wasomi kushiriki katika mradi wa (Sisi na ulezi wa shue), kwa ajili ya kusaidia malezi na ufundishaji vitu ambavyo ndio msingi wa shule, na daraja la kumvusha mtu kutoka katika familia na kumwingiza katika jamii, mazingira ya shule na elimu ndio siri ya mafanikio au sababu ya kufeli, kila jambo la kimaendeleo limetokana na kusoma, hakika kusoma ni jambo muhimu sana, kituo kimechagua mada za kufanyiwa utafiti, nazo ni:

Kwanza: Historia ya shule za kiarabu na maendeleo yake hadi katika zama zetu.

Pili: Falsafa ya malezi ya shule, mada hii itajadili malengo ya malezi na kusoma pamoja na falsafa ya malengo hayo na kinyume chake na uwezekano wa kufikia malengo na njia za kutufikisha kwenye malengo.

Tatu: Misingi ya kuwepo kwa selebasi za masomo, kwa sababu ya tofauti kubwa iliyopo katika selebasi, tutajikita katika selebasi iliyo andikwa na kupitishwa na serikali, pamoja na mwongozo wa mwalimu, sambamba na kuangalia elimu, uwezo na kipaji, pia tutaangalia selebasi zingine na athari zake chanya na hasi (nzuri na mbaya).

Nne: Uongozi wa shule uliopita wasasa na ujao na namna ya kuuboresha kiidara na kimalezi.

Tano: Uandaaji wa walimu katika vyuo vya uwalimu au vitengo vya ufundishaji vilivyopo.

Sita: Njia za ufundishaji na matokeo yake, pamoja na uhusiano wake na maendeleo ya kiteknolojia na yanayo weza kufanywa na teknolojia, na namna ya kutumia teknolojia katika ufundishaji.

Saba: Mwanafunzi ndio nguzo kuu ya elimu na kusoma, mahitaji yake na hatua anazo pitia kimalezi na kielimu, tatizo la maadili na namna ya kupambana nalo.

Nane: Majengo ya shule na ujenzi wake, ujenzi wa madarasa kumbi za mitihani na sehemu za michezo kwa namna ambayo jengo litakua rafiki na mazingira salama kwa msomaji.

Tisa: Changamoto zinazo kabili shule na namna ya kupambana nazo pamoja na uhusiano wa changamoto hizo na mazingira ya vyuo, umuhimu wa kuweka uhusiano baina ya elimu za sekula na elimu za ufundi.

Tafiti za mada hizo tulizo taja hapo juu zitumwe kwenye ofisi ya wahariri, ziambatane na: jina la mada kuu, ni vizuri kutaja rejea, na kuthibitisha kwa kutumia njia maarufu za kisekula. Utafiti hautakiwi kuzidi kurasa (30) zenye maneno (300) kwa kila ukurasa bila kuhesabu rejea, baada ya mada kupasishwa idara itamtaarifu mtafiti na itampa muda wa kukamilisha kazi yake, baada ya mtafiti kumaliza kazi na kuikabidhi katika idara ya wahariri, idara itampa zawadi kwa kuzingatia mambo yafuatayo:

  • - Amana ya kielimu pamoja na kutaja vitabu rejea pembezoni mwa ukurasa (kwenye hamishi) na mwishoni mwa utafiti.
  • - Utafiti uambatane na muhtasari pamoja na mapendekezo yanayo tekelezeka.
  • - Tafiti pamoja na mapendekezo yatumwe kwa wahariri kupitia anuani ifuatayo: css.lb@gmail.com.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: