Kwa kushirikiana Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya: Maukibu ya watu wa Karbala yafanya kumbukumbu ya kifo cha Saidi bun Jubeir (r.a)…

Maoni katika picha
Imefanyika kumbukumbu ya kifo cha Saidi bun Jubeir (r.a) katika malalo yake tukufu, tarehe ya kifo chake inasadifu siku ya leo mwezi ishirini na tano Rabiul Awwal, mawakibu nyingi zimekwenda kuomboleza msiba huu, miongoni mwa mawakibu hizo ni maukibu ya watu wa Karbala ambayo hufanya shughuli zake kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maukibu ya watu wa Karbala ni maukibu ambayo Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimekua zikiisaidia na kushiriki katika harakati zake zote, pia kitengo kimesha fanya mikutano mingi pamoja na viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vilivyopo katika mkoa wa Karbala, kwa ajili ya kufanya tukio hili la maombolezi katika mazingira bora yanayo endana na utukufu wake”.

Akaongeza kua: “Tumeandaa gari za kubeba watu kupitia idara za usafiri za Ataba mbili tukufu, kwa ajili ya kubeba waombolezaji kwenda na kurudi katika mkoa wa Waasit, pamoja na kusaidia baadhi ya utowaji wa huduma katika mawakibu”.

Wakati misafara ya waombolezaji inaendelea kumiminika sauti za vilio na mimbo ya huzuni ilienea, walipo wasili katika haram yake (r.a) wakafanya majlisi ya kuomboleza, na kuimbwa kaswida na mashairi ya huzuni, sambamba na kukumbusha yaliyo wafika watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao watukufu akiwemo Saidi bun Jubeir (r.a).

Kumbuka kua maukibu hii ya kuomboleza hufanywa kila mwaka na watu wa Karbala, kwa ajili ya kukumbuka tukio hili na matukio mengine ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), maukibu mbalimbali za Karbala na vikundi vya Husseiniyya huungana katika kuomboleza msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: