Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud latoa bidhaa mpya yenye upora wa hali ya juu…

Maoni katika picha
Shirika la teknolojia ya kilimo cha kosasa Aljuud ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limetoa bidhaa mpya, nayo ni mbolea yenye ubora mkubwa iitwayo (Mbolea ya Aljuud ya tente za dhahabu), bidhaa hii ni sehemu ya mkakati wa shirika hili unaolenga kuboresha aina mbalimbali za mazao hapa nchini, kwani mbolea ni kitu muhimu katika kuzalisha aina zote za mazao.

Bidaa hiyo imetengenezwa katika viwango vitatu tofauti, ambavyo ni: mbolea ya Botasiyum, mbolea ya hatua zote na mbolea ya Netrojen.

Mbolea ya Botasiyum (40-0-5) inafaida zifuatazo:

  • 1- Inaongeza ukubwa wa tunda.
  • 2- Inatoa matunda mazuri yanayo pendwa sokoni.

Sababu za kutumia mbolea hii ni:

  • 1- Inakuza mimea haraka.
  • 2- Inaathi ukubwa wa matunda (madogo).

Faida za mbolea hii zinapatikana katika hatua zote (25-15-10) kama ifuatavyo:

  • 1- Inaongeza ukubwa wa tende na maharage.
  • 2- Inastawisha shina la mmea.
  • 3- Inajenga protini za mmea.
  • 4- Inaimarisha klorofiil.
  • 5- Inauwezo wa kubadilisha mmea.

Msukumo wa kutumia mbolea hii ni:

  • 1- Mazao kukosa rutuba.
  • 2- Unaweza kuitumia katika umri wowote wa mazao yako.
  • 3- Inaimarisha mizizi na kuiwezesha kufyonza chakula vizuri.
  • 4- Inaongeza mavuno.

Kuhusu mbolea ya Netrojen (0-5-30) faida zake ni kama zifuatazo:

  • 1- Inaongeza ukuwaji wa shina.
  • 2- Inajenga chembechembe za Protini.
  • 3- Inaimarisha Klorofiil.
  • 4- Inauwezo mkubwa wa kuubadilisha mmea.

Msukumo wa kuitumia:

  • 1- Upungufu wa Natrojen.
  • 2- Ukosefu wa rutuba.
  • 3- Mimea kua ya njano.
  • 4- Inaathiri ukubwa wa matunda (madogo).

Kumbuka kua shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud ni moja na mashirika ya Atabatu Abbasiyya tukufu linalo tengeneza vifaa vya kilimo na vifaa vya viwandani hapa Iraq, kama vile: (mbolea, chembechembe hai, majosho na kinga, vifaa tiba na bidhaa za viwandani).

Toghuti ya shirika ni: (info@aljoud-intaj.iq) (www.aljoud-intaj.iq).
Anuani ya shirika ni: barabara ya Karbala – Najafu, mkabala na nguzo namba (1145). Namba za simu za shirika ni: (07801035422) (07728792386) (07721465669) ((07723862460.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: