Kutokana na umuhimu wa kufundisha kazi za ufundi na kujenga uwezo wa wanafunzi, shule ya wavulana Nurul Ameed ambayo ipo chini ya shule za Al-Ameed, asubuhi ya Jumatatu (25 Rabiul Awwal 1440h) sawa na (3 Desemba 2018m) imefanya warsha iliyo ipa jina lisemalo: (Finyanga udongo).
Katika warsha hiyo yametolewa maelezo ya kina kuhusu fani hiyo na historia yake pamoja na namna ya kutengeneza vyombo vya kifahari, imepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanfunzi, wametengeneza vyombo vingi na vya aina mbalimbali.
Warsha hii imefanyika kwa ajili ya kulinda fani hii na kuiendeleza katika taasisi za malezi, pamoja na kuwaonyesha wanafunzi vifaa vya kujifunzia na nyezo muhimu katika kulendeleza fani hii.
Tunapenda kuwakumbusha kua shule za Al-Ameed zipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, zinajitahidi kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ndani ya kipindi chote chwa mwaka wa masomo, chini ya usimamizi wa walimu bora na mahiri.