Msafara wa Alwafaa unaohusika na kutoa huduma za kibinaadamu warejelea kazi zake katika mkoa mtukufu wa Karbala baada ya kusimama kwa muda…

Maoni katika picha
Msafara wa Alwafaa unaohusika na kutoa huduma za kibinaada chini ya kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) leo umeanza kufanya kazi zake katika mkoa mtukufu wa Karbala, baada ya kusimama kwa muda na kushughulika na minasaba ya kidini katika mwezi wa Muharam na Safar.

Ugeni unaowakilisha msafara (hamla) umetembelea familia za mashahidi na majeruhi na kuangalia mahitaji yao sambamba na mazingira wanayo ishi kwa ujumla.

Uongozi wa kikosi hicho siku za nyuma ulitoa wito kwa taasisi na vyombo vya habari pamoja na watu ambao wako tayali kujitolea waungane nao katika msafara wa Alwafaa, ulioanzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu, yakuwasaidia watu hawa watukufu, kwa maelezo zaidi piga simu namba (07706301415).

Tunapenda kukumbusha kua msafara wa Alwafaa ulianzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na watendaji wake wakuu ni kikosi cha wapigani cha Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuzienzi familia za mashahidi na majeruhi, kutokana na kujitolea kwao kwa ajili ya taifa, na kuwapa msaada wa hali na mali kadri ya uwezo wetu, utekelezaji wake unafanyika kwa usawa katika miji na mikoa tofauti, tulianza na mikoa ya kusini kisha tukaenda katika mikoa ya kaskazini lengo letu ni kuifikia miko na miji yote ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: