Nafasi ya Abulfadhil Abbasi na heshima aliyonayo kwa kaka yake Imamu Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Nafasi ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kaka yake Imamu Hussein (a.s) ni jambo la wazi, mara ngapi Imamu Hussein (a.s) alionyesha utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), mwezi tisa Muharam pale jeshi la Umawiyya lilipo taka kuvamia hema zao Imamu Hussein (a.s) alimwambia ndugu yake: (Ewe ndugu yangu wafuate ukawaulize wamekuja na habari gani na wanataka nini?) neno hili linautukufu wake; na linaonyesha utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kaka yake Imamu Hussein (a.s).

Siku ya Ashura Abulfadhil Abbasi (a.s) alipo omba ruhusa ya kwenda kupigana na maadui, Imamu (a.s) alimwambia kua: (wewe ni mbeba bendera wangu, ukiondoka askari wangu watasambaratika), riwaya nyingine inasema kua, alimwambia: (wewe ndio alama ya askari wangu, wewe ndio wingi wa idadi yetu, ukiongoka wingi wetu utatoweka na kusambaratika, na jengo letu litabomoka).

Katika siku ya Ashura alimwambia pia, akiwa amesimama mahala alipo fia, akawa anataka kumpeleka katika hema, Abbasi (a.s) aliapa kwa haki ya babu yake Mtume (s.a.w.w) na kumuomba kaka yake amuache palepale alipo angukia kwa kuhofia maadui wasije kumvamia mbele yake, Imamu akamwambia: (Mwenyezi Mungu akulipe heri, hakika umemnusuru ndugu yako ukiwa hai na baada ya kifo chako).

Akasimama sehemu hiyo huku analia na kufuta machozi yake (a.s) akasema: (hivi sasa mgongo wangu umevunjika, na nguvu zimeniisha, maadui wangu wamefurahi), na mengine mengi aliyasema yanayo onyesha utukufu wa Abbasi (a.s) mbele ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: