Ugeni wa mafundi kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umeanza hatua za kwanza za ukarabati wa malalo ya bibi Ruqayya (a.s) katika mji wa Damaska… Maoni katika picha

Maoni katika picha
Ujumbe wa mafundi uliotumwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji mkuu wa Sirya Damaska, kazi zao hazijaishia katika kukarabati malalo ya bibi Zainabu (a.s) peke yake, bali wamefanya kazi pia ya kukarabati sehemu nyingine tukufu ambayo ni malalo ya bibi Ruqayya (a.s), mafundi hao walianza kufanya upembuzi yakinifu na wakaandika mambo yanayo hitajika katika ukarabati huo.

Ukarabati utafanyika chini ya mwongozo wa idara ya umeme, utahusisha ufungaji wa taa, kuongeza milango itakayo tengenezwa kwa mbao upande wa wanaume na upande wa wanawake, pamoja na kufunga viyoyozi na mfumo wa kamera za ulinzi, sambamba na kufunga taa za rangi katika kubba tukufu bila kusahau kulisafisha dirisha la kaburi tukufu, kazi zingine zitatangazwa baadae.

Kumbuka kua hii sio mara ya kwanza, imetanguliwa na kazi zingine zilizofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia jopo la mafundi waliofanya ukarabati wa aina mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: