Jopo la mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu laanza kutengeneza mfumo wa umeme katika malalo ya bibi Zainabu (a.s)…

Maoni katika picha
Jopo la mafundi kutoka Atabatu Abbasiyya wameanza kufanya marekebisho katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) ndani ya mji mkuu wa Sirya Damaska, chini ya mkakati maalum uliopangwa tangu hatua ya kwanza ya matengenezo haya ambapo walifanya ukarabati katika sistim ya umeme ya malalo matakatifu.

Kiongozi mkuu wa kazi hii ambaye pia ni mkuu wa idara ya umeme chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Ali Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika ni fahari kubwa kwetu kupata fursa ya kukarabati mfumo wa umeme katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), baada ya kuwasili mahala hapa mafundi wetu walianza kazi ya upembuzi yakinifu na kubaini vitu vinavyo hitajika kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa hatua ya kwanza, vifaa vilivyo hitajika vilitengenezwa na wataalamu wetu, navyo ni (konekta) tatu zenye uwezo wa kubeba mb (150) na njia ndogo (18), zinazo washa taa za sehemu mbili za uwanja wa haram tukufu kwa utaratibu maalumu baada ya kua hapo awali kulikua hakuna utaratibu maalum”.

Akaongeza kua: “Pamoja na kazi hizi, kuna kazi zingine zimefanyika pia, kama vile kubadilisha taa za zamani katika uwanja wa haram tukufu, taa za wat (240), nazo hukaa muda mrefu na hazitumii umeme mwingi na zinamwanga mzuri, pia taa mbovu zimetolewa na kuwekwa mpya, vilevile tumeongeza mapambo ya maumbo ya nusu duara pamoja na alama za Atabatu Abbasiyya za (kiganja) pamoja na taa maalumu zitakazo fungwa kwenye madirisha ya kubba tukufu kwa nje”.

Kumbuka kua idara ya umeme ya Atabatu Abbasiyya tukufu inauwezo na uzowefu mkubwa wa kazi hizi, wametengeneza upya mfumo wa umeme, walianza na kukarabati chumba cha kituo cha usambazaji wa umeme, baada ya kua hapo uwali umeme ulikuwa hauna mfumo maalum, sasahivi malalo ya bi Zainabu (a.s) yanaumeme usio zimika na yameunganishwa na vituo viwili vikuu vya umeme.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: