Mfumo wa (Nahwul Qamaru) ni taa liangazalo katika sekta ya malezi na elimu na nimfumo pekee katika michezo ya watoto hapa Iraq…

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu cha Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kianze kufanya kazi kimelipa umuhimu mkubwa swala la malezi na kujenga kizazi cha watu wenye uwezo wa kujenga taifa, imetumia uwezo wake wote katika kuhakikisha hilo, wameweka ratiba mbalimbali za masomo na michezo, wamefikia kuunda mfumo mmoja wa michezo unayo shughulikia michezo ya watoto wa shule za msingi, maahadi na vyuo, miongoni mwa mifumo iliyo towa mafanikio na kukubalika ni mfumo wa (Nahwul Qamaru), umekua taa liangazalo katika sekta ya elimu na malezi, nao ni mfumo wa pekee hapa Iraq.

Mfumo wa (Nahwul Qamaru) unatumika rasmi kwa wanafunzi wa shule za Al-Ameed, unahusisha vitu mbalimbali (mafundisho ya dini, lugha, tabia, sayansi, kiengereza, na vinginevyo), umeandaliwa na jopo la wataalamu waliobobea katika sekta ya malezi na elimu ya juu.

Mfumo huu ni taa linalo angazia elimu na michezo ya watoto, nao ni mfumo wa kwanza maalumu unaolenga kuwajenga watoto katika mambo mbalimbali.

Kumbuka kua mfumo huu unahusisha hatua mbalimbali za kuwaandaa wanafunzi na unaendana na umri pamoja na uwezo wa akili za watoto, wanafundishwa vitu vingi vya msingi kwa kutumia njia za michezo sambamba na kuboresha sekta ya michezo katika shule za Al-Ameed.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: