Jopo la mafundi kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu waliotumwa kuja kufanya matengenezo katika malalo mawili matukufu, malalo ya bibi Zainabu na bibi Ruqayya (a.s), wameanza kazi rasmi katika malalo ya bibi Ruqayya (a.s), baada ya kufanya upembuzi yakinifu na kubaini sehemu zinazo takiwa kufanyiwa matengenezo na kukamilika maandalizi yote.
Kwa mujibu wa maelezo ya watendaji wa mradi huo, matengenezo yamehusisha ufunikaji katika milango ya wanawake, eneo linalo kadiriwa kufika mita (500) za mraba, sehemu hiyo imefunikwa kwa umaridadi mkubwa na yamewekwa mapambo yanayo endana na utukufu wa eneo hilo, pamoja na kufanana na mapambo yaliyopo, pia wamefunga viyoyozi vyenye uwezo mkubwa wa kutia baridi sambamba na kufunga mfumo wa umeme na kuunganishwa na mfumo mkuu wa malalo hii, pamoja na kazi zingine kuhusu dirisha tukufu na kuta za haram pamoja na kukarabati mfumo wa umeme na kuweka taa mpya sambamba na kuweka mfumo wa sauti (spika) na kamera.
Kumbuka kua hii sio mara ya kwanza Atabatu Abbasiyya kufanya marekebisho katika malalo hizi, wamesha fanya ukarabati mara nyingi.