Kwa mahadhi ya Iraq na Misri: Arshu Tilaawah yafanya hafla yake ya kila wiki…

Maoni katika picha
Kuna miradi mingi ya Qur’ani inayo endeshwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilaawah, ni mradi unaokusudia kunufaika na vipaji wa usomaji wa Qur’ani vilivyopo Iraq na kuvidhihirisha katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na kuendelea kulea vipaji hivyo chini ya utaratibu maalumu na usimamizi wa walimu wabobezi.

Miongoni mwa vipengele muhimu vya mradi huu ni kufanya hafla za usomaji wa Qur’ani kila wiki ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na hushirikisha wasomaji kadhaa wa mradi huu pamoja na walimu wao, hafla hii inawasomaji wa mahadi ya Iraq na Misri, kwanza walisoma kwa mahadhi ya Iraq bwana Hussein Hamiid Juburi na Mauhubu Hussein Rikabi ambao ni wasomaji wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdad, kisha wakasoma kwa mahadhi ya misri bwana Liith Ubaidiy ambaye ni msomaji wa Atabatu Abbasiyya na bwana Hussein Muhammad Shalaal mmoja wa mahafidhi wa tawi la Maahadi la Bagdad.

Mazuwaru watukufu pia wameshiriki katika hafla hii, wamesikiliza na kutafakari aya za Qur’ani tukufu zilizo somwa, sambamba na wale waliangalia moja kwa moja kupitia chanel ya Karbala ya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: