Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaendelea na kazi ya ukarabati katika malalo ya bibi Zainabu (a.s)…

Maoni katika picha
(Watumishi wa malalo mawili ya Abulfadhil Abbasi na dada yake bibi Zainabu (a.s) na mazuwaru wao ni fahari kwetu), hiyo ni kauli mbiu ya jopo la mafundi waliotumwa na Atabatu Abbasiyya kuja kufanya matengenezo katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), bado wanaendelea na kazi chini ya ratiba waliyo jiwekea, madhumuni ya kazi hii ni kuhakikisha sehemu hii inakua na muonekano mzuri pamoja na mazingira rafiki yatakayo wawezesha mazuwaru kufanya ibada kwa amani na utulivu.

Kiongozi wa jopo la mafundi na msimamizi wa kazi hii bwana Hussein Hilali ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafiil kua: “Sisi tunaendelea kufanya kazi iliyo tuleta kwa siku ya tano mfululizo, tumefanya ukarabati katika chumba cha mitambo ya spika na kuweka vipaza sauti sehemu mbalimbali, na kuviunganisha na mitambo iliyopo, kwa ajili ya kuhakikisha sauti inafika sehemu kubwa zaidi pamoja na kubadilisha spika zilizo kuwepo katika minara na kuweka mpya zenye uwezo mkubwa sambamba na kuzifanyia majaribio ambapo zimeonyesha uwezo mkubwa”.

Akaongeza kua: “Kuhusu ukarabati wa umeme, tumebadilisha taa za zamani zilizakuwepo katika minara miwili na kuweka taa mpya zenye mwanga mzuri na haziharibiki kwa unyevunyevu wala maji kiasi cha taa (210) katika eneo lenye urefu wa zaidi ya mita (70), hali kadhalika tumemaliza kazi ya kusafisha na kubadilisha taa za mapambo na kuzifanya zing’ae na kuangaza vizuri juu ya kaburi tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Tumebadilisha betrii la mtambo wa kuinulia vutu ulioletwa siku za nyuma na kukabidhiwa uongozi mkuu wa bibi Zainabu (a.s), pamoja na kufanya kazi ya kusafisha dirisha la malalo tukufu kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo hutumika kusafishia malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kupuliza uturi (marashi) yenye harufu nzuri inayo endana na harufu ya mwenye malalo hii takatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: