Kwa ushiriki wa watu 1000: Maahadi ya Qur’ani tukufu kitengo cha wanawake yahitimisha mashindano ya kitaifa ya pili

Maoni katika picha
Watu (1000) kutoka mikoa tofauti ya Iraq wameshiriki katika mashindano ya Qur’ani, baada ya kumaliza hatua za mchujo walipatikana watu (85) waliofaulu kuingia katika mashindano ya kuhidadhi Qur’ani tukufu, Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Ataba tukufu lilihitimisha mashindano ya awamu ya pili ya kuhifadhi Qur’ani tukufu, yanayokusudia kueneza utamaduni wa Qur’ani na kuimarisha uhusiano na kutabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, na kuitambua nafasi ya Qur’ani katika maisha ya kila siku, mashindano haya ni njia ya kushajihisha usomaji wa Qur’ani tukufu na kuihifadhi pamoja na kufanya mazingatio katika aya tukufu, vikao vya mwisho vya mashindano vilivyo dumu siku tatu vilikua na washiriki waliohifadhi juzuu tatu, juzuu tano, juzuu kumi, juzuu kumi na tano, juzuu ishirini na waliohifadhi Qur’ani yote.

Kikao cha mwisho kilicho fanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) kilikua na ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na naibu katibu mkuu Mhandisi Bashiri Muhammad Jaasim Rabiiy, amepongeza kufanyika kwa mashindano haya yaliyo simamiwa na Maahadi tawi la wanawake, kwani yanaimarisha usomaji wa Qur’ani na wanawake na kuwawezesha kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, akawapongeza washindi wa mashindano haya na akawataka waendelee kukitumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Hafla ilipambwa na usomaji wa Qur’ani wa vikundi kutoka kwa vijana wa marafiki wa Alkafeel (Ahbaabul Kafeel) ambao walisoma surat Fajri, kisha yakatangazwa majina ya washindi na wakapewa zawadi pamoja na kuizawadia kamati ya majaji, pia klikua na zawadi ya haafidhi bora wa Qur’ani tukufu kutoka katika Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake, washindi waligawanyika sehemu zifuatazo:

  • - Tisa waliohifadhi Qur’ani nzima.
  • - Kumi waliohofadhi juzuu ishirini.
  • - Sita waliohifadhi juzuu kumi na tano.
  • - Kumi waliohifadhi juzuu kumi.
  • - Ishirini na nne waliohifadhi juzuu tano.
  • - Ishirini na saba waliohifadhi juzuu tatu.

Nafasi za washindi walioshiriki shindano la kitaifa la kuhifadhi Qur’ani nzima ni:

Nafasi ya kwanza: Maryam Ali Khalfu

Nafasi ya pili: Sara Rahim Jabbaar.

Nafasi ya tatu: Laila Muhammad Ali Abdu.

Waliohifadhi juzuu ishirini:

Nafasi ya kwanza: Farduus Najaah Saalim.

Nafasi ya pili: Istabraq Abdul-Amiir Abduridha.

Nafasi ya tatu: Ilaaf Swabiih Twalibu.

Waliohifadhi juzuu kumi na tato:

Nafasi ya kwanza: Dhuha Hussein Halo.

Nafasi ya pili: Aamaali Abduzahara Khaliwi.

Nafasi ya tatu: Zainabu Mujad Swahibu.

Waliohifadhi juzuu kumi:

Mshindi wa kwanza: Zaharaa Faalih Abiis.

Mshindi wa pili: Jannat Adnani Haadi.

Mshindi wa tatu: Nagham Rasuul Aufi.

Waliohifadhi juzuu tano:

Mshindi wa kwanza: Batuli Qassim Muhammad.

Mshindi wa pili: Swafa Muhammad Hussein.

Mshindi wa tatu: Rihana Ali Hashim.

Wasiohifadhi juzuu tatu:

Mshindi wa kwanza: Rihana Mustafa Naajih.

Mshindi wa pili: Zainabu Muhsin Jabbaar.

Mshindi wa tatu: Istabraq Muhammad Aliwi
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: