Balozi wa Uturuki nchini Iraq bwana Faatih Yaldaz amesema kua; hakika hospitali ya rufaa Alkafeel pamoja na kuwa haina muda mrefu tangu ianzishwe tayali imesha onyesha mafanikio makubwa, na imewaonyesha wairaq kua wanaweza kutoa huduma za matibabu zenye viwango vya kimataifa kwa raia wa Iraq, sisi waturuki tunaona fahari kubwa kwa jambo hili kwani tumekuwa wadau wa hospitali hii tangu mwanzo.
Ameyasema hayo katika hafla iliyo endeshwa na hospitali hiyo kufuatia kufanikiwa kwa ubasuaji wa moyo wazi ambao unafanywa na hospitali hiyo kwa miaka miwili sasa, akaongeza kusema kua: “Nijambo zuri kwetu kuwepo katika mji huu mtakatifu, waislamu wa Uturuki wanauhusiano mkubwa na mji huu pamoja na mapenzi ya hali ya juu kwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), hili sio jambo geni kwao, kwani wamelelewa katika mapenzi hayo, hakika mji wa Karbala ni mji mtukufu zaidi kwetu, na wakazi wa mji huu wananafasi ya pekee katika nyoyo zetu”.
Akabainisha kua: “Hospitali hii inautukufu wa pekee katika nyoyo zetu kwa sababu imefungamana na Atabatu Abbasiyya tukufu, sisi waturuki tunajitahidi kuwasaidia ndugu zetu kwa uwezo wetu wote, katika kila jambo linalogusa maisha yao ikiwa ni pamoja na sekta ya tiba na afya, na tunajifaharisha kwa madaktari wetu wanaofanya kazi pamoja na madaktari wa Iraq, tunatamani kuwepo kwa hospitali kama hii katika kila mkoa wa Iraq”.
Akaendelea kusema kua: “uhusiano wa waturuki wa wairaq hauishii katika mambo ya kiuchumi pekeyake, bali kuna uhusiano wa kitamaduni na kihistoria pia, uhusiano huo ndio chachu ya kutupeleka katika ushirikiano wa mambo mengine pia, kama leo hii tunavyo shirikiana katika sekta ya afya, hatubebi tu wagonjwa wa kiiraq na kuwapeleka Uturuki au kuleta madaktari wa kituruki hapa Iraq, bali tunafanya kazi ya kuwajengea uwezo wairaq wawe sawa na waturuki bali wawashinde hata waturuki, tutaendelea kufanya kila tuwezalo katika kuimarisha uhusiano baina wa wairaq na waturuki”.