Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chatoa kozi ya lugha ya kifarsi kwa watumishi wake

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuboresha huduma na kukuza uwezo wa kifikra na kiutamaduni ambapo kujua lugha ya mtu ni miongoni mwa msingi mkubwa wa mambo hayo, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu chatoa kozi ya kujifundisha lugha ya kifarsi kwa watumishi wake, nayo ni sehemu ya kozi nyingi ambazo huwapa watumishi wake.

Kozi hii ambayo inasimamiwa na idara ya lugha ya chuo kikuu cha Alkafeel itadumu kwa muda wa miezi sita, kila wiki watasoma siku tatu, inalenga kuwawezesha kusoma, kuandika na kuongea lugha ya kifarsi, mwishoni mwa kozi hii watapewa mtihani na wale watakao faulu watapewa vyeti kutoka chuo kikuu cha (Farduusi) kilichopo katika mji mtukufu wa Mash-hadi, ua kutoka wizara ya elimu ya Iran.

Washiriki wameonyesha kufurahia sana kozi hii, kwa sababu inawajengea uwezo wa lugha na kurahisisha mawasiliano baina yao na mazuwaru wa mji mtukufu wa Karbala.

Kumbuka kua kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kinaendelea kutoa semina za kuwajengea uwezo watumishi wake katika mambo mbalimbali wanayo hitajia, hapo awali walipewa kozi ya kompyuta, kupiga picha, maendeleo ya binaadamu, lugha ya kiarabu na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: