Mahudhurio makubwa ya wadau wa Qur’ani: Mradi wa (Mimbari zenye nuru) unaendelea na mahafali za Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya inamiradi mingi ya Qur’ani inayo lenga kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa (Mimbari zenye nuru) ambao unasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani cha Maahadi, nao unahusisha uendeshaji wa vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani na nje ya mkoa wa Karbala, katika Ataba tukufu au mazaru takatifu na katika husseiniyya na misikiti, chini ya wasomaji mahiri wa Qur’ani kutoka ndani na nje ya Iraq kwa kufuata ratiba maalum.

Kituo hiki kimefanya mahafali ya usomaji wa Qur’ani katika wiki ya tatu huko Bagdad, kufuatia maombi ya taasisi za Qur’ani, kikao hiki kimefanywa kwa kushirikiana na Madrasa ya Aswihabul-Kisaa ya maarifa ya Qur’ani, ambayo ipo chini ya taasisi ya Athaqlu-Akbaru katika mji wa Bagdad, na kuhudhuriwa na waumini wengi sana, wasomaji walisoma kwa mahadhi mazuri sana, nao ni msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Faiswal Matwar na bwana Ahmadi Jaabiri, pamoja na washiriki wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa na wanafunzi wa madrasa ya Aswihabul-Kisaa ambao ni Ahmadi Mithaaq na Sajjaad Hassan, pia kulikua na ujumbe kutoka katika taasisi ya Athaqlu-Akbaru ulio wasilishwa na Dokta Fahariy Akili, alisifu miradi inayofanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu na jinsi inavyo saidia sekta ya Qur’ani, akasisitiza kua Maahadi iko mstari wa mbele daima katika kufundisha uwelewa wa Qur’ani katika mambo mbalimbali, akaelezea vilevile harakati zinazofanywa na taasisi yao katika sekta ya Qur’ani.

Kumbuka kua mradi wa (Mimbari zenye nuru) umejikita katika kuendesha vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mikoa yetu mitukufu pia ni moja ya miradi inayofanywa kwa kushirikiana baina ya kituo cha miradi ya Qur’ani na taasisi mbalimbali pamoja na vituo vya Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: