Dirisha la khutuba za Ijumaa katika mtandao wa kimataifa Alkafeel ni marejeo ya uhakika

Maoni katika picha
Ni wazi kwa kila mtu kuwa khutuba za Ijumaa zinazo tokana na Marjaa Dini mkuu na kutolewa na wawakilishi wake katika mji wa Karbala kwenye mimbari ya swala ya Ijumaa inayo swaliwa ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussei (a.s) zina umuhimu mkubwa, macho ya walimwengu wote hususan raia wa Iraq huelekezwa Karbala kufuatilia khutuba hizo, zilizojaa mafundisho ya dini, aqida, mambo ya kijamii na mengine mengi yanayo husu maisha yao, khutuba hizi maranyingi zinazungumzia kila jambo lenye manufaa nao, Marjaa Dini mkuu ni baba wa kiroho wa wairaq wote wa dini, madhehebu na tabaka zote.

Kutokana na umuhimu wa khutuba hizo, idara ya intanet ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel umeweka dirisha (ukurasa) maalumu wa khutuba za Ijumaa kwa lugha zote za mtandao ambazo ni (kiengereza, kifarsi, kiurdu, kijerumani, Kiswahili na kifarsi -bila kusahau lugha mama ya kiarabu-), ukurasa huo unakhutuba ya maandishi, kuangalia na kusikiliza, pamoja na mada kuu zikienda sambamba na vipengele muhimu vya khutuba ya kwanza na ya pili, baada ya ukurasa huu kudumu kwa miaka mingi, umekua chanzo muhimu kielimu cha habari katika vyombo vya habari vinavyo rusha au kuripoti khutuba za Ijumaa, ukurasa huu unakhutuba zoto kuanzia khutuba ya kwanza iliyotolewa mwaka (2003) hadi khutuba ya mwisho kutolewa, kila wiki huongezwa khutuba mpya katika ukurasa huo.

Sifa pekee ya ukurasa huu ni kupatikana kwa khutuba yote, hii ndio tofauti kubwa iliyopo katika mtandao wa Alkafeel na mitandao mingine ya habari, mtandao huu unampa mtazamaji khutuba kamili na kwa njia tofauti, kwa njia ya video yenye ubora mkubwa au kusoma au kusikiliza sauti, jambo hili limechangia kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi, kwani wanapata wanacho hitaji, iwe ni maandishi, sauti au video, khutuba hizo zinapatikana kupitia anuani ifuatayo: https://alkafeel.net/inspiredfriday/archive.php
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: