Maoni katika picha
Limefanyika hilo katika kikao cha ibada zinazo fanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya Jumanne na Alkhamisi ya kila wiki, Jumanne hii imesadifu (2 Rabiul Thani 1440h) sawa na (10 Desemba 2018m), ibada hizi zimeenda sambamba na kumbukumbu ya tangazo la ushindi wa Iraq dhidi ya genge la ujinga na dhulma la Daesh, uliopatikana kupitia jeshi letu shupavu na Hashdi watukufu, baada ya kufanya ziara maalumu kwa mwenye malalo na kusoma wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu uitwao (Lahnul-Ibaa), waliimba mimbo na kaswida za ushujaa kutokana na ushindi wa raia wa Iraq, wakajikumbusha ushujaa na ujasiri waliojifunza kutoka kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), uliopewa baraka na Marjaa Dini mkuu pale alipotoa fatwa tukufu ya kujilinda itakayo kumbukwa milele na kubakia katika vichwa vya vizazi na vizazi.
Wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awarehemu mashahidi wa Iraq, ambao damu zao zimemwagika katika ardhi ya Iraq kutokana na njama za maadui, na wakamuomba awaponye haraka majeruhi wote, wakawaombea dua ndugu zao waliopo katika uwanja wa vita tangu siku ya kwanza hadi sasa, wameomba dua wakiwa pembeni ya kaburi tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s), na huo ndio msaada mkubwa kwa ndugu zao wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi, mbali ya misaada ya hali na mali ambayo wanaendelea kutoa katika vikosi mbalimbali vya wapiganaji na sehemu tofauti.