Mwaka mmoja baada ya ushindi… mazingatio, matukio na ukweli wa kihistoria

Maoni katika picha
Fatwa + Mwitikio wa raia wa Iraq = Ushindi dhidi ya Daesh.

Ushindi wetu dhidi ya Daesh ------- umeihifadhi Iraq na nchi za kieneo zisiangamie.

Ushindi wetu dhidi ya Daesh ------- umetokana na uimara wa jeshi, ujasiri wa askari wake na kikosi cha kupambana na ugaidi + kuongezeka kwa ari na mwamko wa raia wake.

Ushindi wetu dhidi ya Daesh ------- umetokana na kuanzishwa kwa jeshi la kiraia la pili kwa nguvu Duniani + na kuongezeka kwa kiwango cha uwezo wa kupambana na ugaidi hadi kufikia nafasi ya (12) Duniani.

Kujitolea ndio kulikoleta ushindi na asilimia kubwa ya waliojitolea ni watu wa kusini na katikati ya Iraq ------- kulisaidia kutambua ukweli wa magaidi wa Daesh na mashekhe wa fitna katika mkoa wa Nainawa, Ambaar na Swalahu-Dini walio wahofisha watu wao kutokana na madai ya hatari ya mashia (kama njia ya kutengeneza fitna).

Wairaq kupata ushindi ndani ya miaka mitatu na nusu ------- na kuumaliza mpamgo wa kimataifa wa kufuta taifa la Iraq na kubakia Daesh miaka (30)!!!!.

Fatwa + mwitikio wa wairaq wa fatwa hiyo + jinai za Daesh katika miji waliyo iteka + huruma ya watu walioitikia fatwa kwa ndugu zao wanaoishi katika miji hiyo + msaada wa mawakibu + harakati za kamati ya kusaitia wakimbizi katika ofisi ya Marjaa Dini mkuu + juhudi za Ataba katika kutoa misaada = (vimesaidia) kufuta mitazamo mibaya iliyo pandikizwa na magaidi dhidi ya shia kupitia mashekhe wa fitna katika miji iliyotekwa na Daesh au Alqaaida kwa muda wa miaka (13) kama vile mji wa Faluja.

Sababu kuu za ushindi

Ushindi umepatikana kutokana na sababu kuu mbili kama zilivyo tajwa na Marjaa katika khutuba mbalimbali.

Sababu kuu zilizo leta ushindi ni:

Kwanza… Marjaiyya

Kutokana na mambo yafuatayo:

  • a- Kuwaelezea wanajeshi wa serikali fatwa ya jihadi dhidi ya magaidi (10/6/2014).
  • b- Fatwa ya jihadi ya kutoshelezeana (jihadul-kifaya) kwa kila mtu mwenye uwezo wa kubeba siraha (13/06/2014).
  • c- Kazi zinazofanywa na kamati ya kusaidia familia za mashahidi iliyopo katika ofisi yake ambayo imesha tumia mabilioni ya hela na bado inaendelea kutoa misaada hadi sasa.
  • d- Kazi zinazofanywa na taasisi ya Ain inayojihusisha na kulea jamii, inayo msaidia kila yatima aliyetokana na fatwa ya kujilinda au kitendo cha ugaidi wa Daesh.
  • e- Kazi zinazofanywa na kamati ya kusaidia wakimbizi ambayo ipo katika ofisi ya Marjaa Dini mkuu.
  • f- Wanafunzi wa hauza na viongozi wa wapiganaji walio uwawa makumi kwa makumi na wengine wengi kujeruhiwa.
  • g- Kamati ya daawah, ambayo ilipeleka makumi ya mubalighina katika uwanja wa vita kwa ajili ya kuwanasihi na kuwajenga kiimani wapiganaji, na wao pia ni miongoni mwa waliopata shahada (uwawa).
  • h- Kamati ya kusaidia wakimbizi ya Ataba tukufu, ilisaidia maelfu ya wakimbizi katika mikoa ya Nainawa, Swalahu-Dini na Ambaar.
  • i- Kazi za kamati za Ataba za kulea familia za mashahidi na majeruhi sambamba na kutibu mamia ya majeruhi bure katika hospitali za Ataba.
  • j- Maelekezo yaliyokuwa yanapatikana katika khutuba mbili za Ijumaa kwa wapiganaji kila wiki, kipindi chote cha vita iliyo chukua siku (1275).

Pili … raia wa Iraq

Kutokana na mambo yafuatayo:

  • a- Mwitikio wa wairaq kuhusu fatwa, kwanza jeshi la serikali liliitikia vizuri fatwa hiyo, pili raia walijitokeza kwa wingi, karibu asilimia (%55) ya wairaqi wenye uwezo wa kubeba siraha walijitokeza ndani ya siku mbili tu, nayo ni idadi kubwa zaidi ya raia waliokua tayali kujitolea katika vita duniani katika historia. Kisha wakaanza kuunda vikosi vipya vya askari na wengine wakajiunga katika vikosi vilivyo kuwepo, wote kwa ujumla waliunda kikosi kinacho itwa Hashdi Sha’abi na kukiweka chini ya usimamizi wa serikali, pamoja na kulinda haki ya kila aliyejiunga katika vikosi vya kikoo kutokana na msukumo wa fatwa na kumuhesabu kama mpiganaji huru. Wote hao Marjaa Dini mkuu aliwaambia kua:

“Napenda kusisitiza kuwa mwenye ubora na utukufu mkubwa katika vita hii iliyodumu miaka mitatu, ni wapiganaji shujaa wa vikosi vyote”

Akasema: “Hakika Marjaa Dini mkuu aliye toa fatwa ya kujilinda… haoni kama kuna yeyote anaye karibia utukufu wenu katika kufanikisha ushindi huu wa kihistoria”.

Akasema: “Kama sio mwitikio wenu wa fatwa na kupigana kwenu kwa ushujaa na ujasiri katika uwanja wa vita katika kipindi cha zaidi ya miaka mitatu ushindi huu usingepatikana”.

  • b- Mawakibu zilisaidia kutoa chakula, vinywaji, mavazi na misaada mingine mbalimbali kwa wapiganaji wa kujitolea na waserikali katika uwanja wa vita na kwenye mazingira magumu sana yaliyo pelekea kupata shahada (kuuwawa) watumishi wa mawakibu na wengine kujeruhiwa.
  • c- Kazi kubwa iliyofanywa na jeshi la serikali na kikosi cha umoja wa kupambana na magaidi.
  • d- Kazi kubwa iliyofanywa na vikosi vya wapiganaji vya Ataba vilivyo undwa baada ya fatwa.
  • e- Kazi kubwa iliyofanywa na viwanda vya kijeshi na vya serikali ya Iraq.
  • f- Kazi iliyofanywa na familia za walioitikia wito wa Marjaiyya kwa kuwahamasisha watoto wao kuingia vitani, na kusaidia kuwalea mayatima na wajane.
  • g- Kuungana kwa koo za wairaq kwa ajili ya kuhakikisha wanapata ushindi.

Sababu zingine za ushindi.

Mambo haya yamesaidia pia kupatikana ushindi:

Shukrani za pekee ziwaendee waliotusaidia kwa kutuuzia siraha na waliokubali kuwa washauri wa askari wetu, na wale waliotupa taarifa za kweli dhidi ya Daesh wakati wa mapambano!!!.

Tunatoa shukrani kwa kila aliyechangia kwa namna yeyote ile ushindi huu…

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwa ushindi huu..

Marjaa pia aliwashukuru:

“Marafiki wote waliosimama pamoja na Iraq katika mtihani wa vita dhidi ya Daesh, na wakawasaidia wananchi wa Iraq, na akamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awaepushe na kila aina ya shari na awape amani na utulivu”.

Kila mwaka na Iraq pamoja na raia wake wawe na kheri nyingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: