Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambao ndio watekelezaji wakuu wa mradi huu, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Eneo linalozunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni dogo, katika siku za ziara huwa kunamsongamano mkubwa, hasa kwenye barabara inayo elekea katika mlango wa Kibla, ambao hutumiwa pia kwa kuongozea swala za jamaa katika siku za Ijumaa na kipindi cha ziara, baada ya kupewa jukumu la kuoneza eneo la mlango huo mafundi wetu walianza kufanya kazi zifuatazo:
- - Kuondoa wigo wa bustani.
- - Kuhamisha mauwa na udongo maalumu uliokuwepo katika bustani hiyo na kupelekwa katika vitalu vya Alkafeel kwa kusaidiana na wataalamu wa vitalu hivyo.
- - Kuchimba sehemu iliyokuwa ya bustani kwa kiwango fulani.
- - Kurekebisha njia za umeme na maji zinazo pita eneo hilo.
- - Kuweka kokoto (Sabbiis).
- - Kusawazisha sehemu iliyo ongezwa.
- - Kumwaga zege.
- - Kusawazisha ukuta wa chuma uliokatwa katika bustani kwa namna ambayo hauta athiri muonekano wake.
Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi ni moja ya vitengo vyenye msaada mkubwa katika maendeleo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na hubeba jukumu la ujenzi na ukarabati wa vitu mbalimbali, kama kukarabati vyoo vya Ataba tukufu na vitu vinavyo fungamana navyo, pamoja na mambo ya usanifu na ujenzi wa miradi mingi inayofanywa na Ataba tukufu.