Miongoni mwa harakati za shule za Al-Ameed ambazo zipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kufuatia kumbukumbu ya kumaliza mwaka tangu Iraq ipate ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, baadhi ya wanafunzi wa shule ya Saaqi na shule ya msingi Al-Ameed ya wasichana, asubuhi ya jana Jumanne (3 Rabiul Thani 1440h) sawa na (11 Desemba 2018m) wametembelea makao makuu ya kikosi cha Abbasi (a.s) na baadhi ya familia za mashahidi wa Hashi Sha’abi, kwa ajili ya kuwajulia hali na kuwarehemu mashahidi pamoja na kuwapa zawadi majemedari hao huku wakiwabebea maua.
Mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadhi Maitham Zaidi alionyesha furaha kubwa kwa kutembelewa, alitoa pongezi nyingi kwa kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, alisema: “Shukrani nyingi ziuendee uongozi wa shule pamoja na kitengo cha malezi na elimu ya juu na wasimamizi wote wa shule hizi tukufu, hakika ziara hii inatupa moyo, tulitoka kupigana na magaidi wa Daesh kwa ajili ya hawa wanafunzi ambao ndio wajenzi wa taifa”.
Akaongeza kua: “Kuja kwa wanafunzi hawa kutoa zawadi na pongezi kwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi ambao walikua sehemu ya walioleta ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, sambamba na wapiganaji wa vikosi vingine, ziara hii inatutia moyo na kutushajihisha zaidi kuendelea kulinda taifa hili kwa hali na mali na kuhakikisha hakuna athari yeyote ya ubaguzi na ugaidi”.