Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud lazindua bidhaa ya meno (kuoshea mdomo) yenye ubora mkubwa

Maoni katika picha
Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limezindua bidhaa mpya iitwayo (Refresh), kwa ajili ya kuoshea mdomo yenye ubora wa hali ya juu. Uzindizi wa bidhaa hii unatokana na haja kubwa iliyopo duniani ya kulinda meno, bidhaa hii ni njia bora zaidi ya kulinda meno na kinywa, inafaida nyingi, madaktari wa meno wanashauri mtu aitumie kila siku.

Bidhaa iliyo zinduliwa na shirika la kilimo cha kisasa Aljuud inaubora mkubwa, imetengenezwa kwa malighafi za dawa na chakula, haina kemekali zozote, inaharufu za aina tatu, harufu ya maua ya rozi, harufu ya maua na’anaa za kulimwa na na’anaa pori.

Kumbuka kua shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limekua na mafanikio makubwa katika kutengeneza visafishio na kinga na kushuhudiwa na kila mtu, katika maonyesho ya kimataifa yaliyo fanyika Bagdad wamepewa pongezi nyingi sana kutoka kwa watu waliotembelea maonyesho hayo kutokana na ubora wa bidhaa zake.

Toghuti ya shirika ni: (www.aljoud-intaj.iq) (info@aljoud-intaj.iq) Ofisi za shirika zipo barabara ya (Karbala – Najafu) mkabala na nguzo namba (1145), namba za simu za shirika ni: (07723862460) (07721465669) (07728792386) (07801035422).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: