Idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea na mradi wa kulinda amani katika majengo ya Abbasi (a.s) ya makazi

Maoni katika picha
Kupitia mafundi wanaofanya kazi katika idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo cha miradi, hivi karibuni wamekamilisha ufungaji wa kamera za ulinzi katika nyumba za makazi za Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuimarisha usalama kama ilivyo katika majengo na taasisi zote za Ataba tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya mawasiliano Muhandisi Farasi Abbasi Hamza: “katika mradi huu zimefungwa takriban kamera (65) zenye uwezo mkubwa, kupitia kamera hizo majengo yote yatakua salama”.

Akaongeza kua: “Ufungaji wa kamera ulipitia hatua kadhaa, kwanza tulifunga nyaya maalumu kwa ajili ya mtandao wa kamera, tukazifunika kwa kitu kinacho itwa (Tarikibil) ili ziwe na muonekano mzuri, kisha tukafunga kamera, halafu ikafuata hatua ya kuziwasha na kuzifungia (DVR) kifaa cha kurekodi picha, na mwisho tukafunga screen, na tukaandaa chumba maalumu cha mitambo na usimamizi mkuu wa kamera hizo, kinacho simamiwa na mafundi waliobobea katika kazi hiyo saa (24) kiala siku”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: