Idha’atu-Riyahaini sauti ya mtoto wa kiislamu yamaliza miaka nane tangu kuanzishwa kwake

Maoni katika picha
Miongoni mwa sehemu za Idhaa ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu na kujihusisha na tabaka la watoto kupitia Idha’a-Riyahaini, inayo rusha matangazo yake kupitia masafa ya Idha’atul-Kafeel, imefanikiwa kuingia katika nyoyo na akili za familia nyingi za watu wa Karbala na kwenye mikoa inako sikika, kwani ni Idhaa pekee iliyo jikita katika malezi ya watoto na kuwajengea uwelewa wa Dini ya kiislamu kwa mujibu wa mwenendo wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Idhaa hii imemaliza miaka nane na sasa inawasha mshumaa wa kuingia mwaka wa tisa, mwaka huu utakua ni mwendelezo wa mazuri yaliyo fanywa katika miaka iliyo pita, na safari ya kuelekea kwenye mafanikio zaidi kwa kuanzisha vipindi vipya vyenye umuhimu mkubwa kwa makuzi ya watoto, vipindi vya Idhaa hii vimewafanya watoto watulie nyumbani kwa ajili ya kuvisikiliza na kuliwazika na mada mbalimbali zinazo zungumzwa, pamoja na vipindi vinavyo rekodiwa kama vile (hadithi ya bibi mwaminifu, Hadithi ya ammi Hassan, Mwenyezi Mungu anamajina mema, hazina ya elimu, funga ya mbaiwai na hazina za herufi) na vinginevyo vingi.

Idha’atu-Riyahaini inapendwa sana na watoto, kwa sababu inavitu vingi vinavyo endana nao na vinavyo onyesha uwezo wa watoto katika mambo mbalimbali na kuwapa nafasi ya kutoa maoni na kusaidia kusambaza uislamu wa kweli na fikra za Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kua pamoja na mafanikio makubwa ya Idhaatul-Kafeel ilikua lazima ifungue kipindi kingine kinacho husu watoto wakiislamu, ndipo ikafungua kipindi kwa jina la Idha’atu-Riyahaini chenye mada mbalimbali zilizo rekodiwa na mubashara (moja kwa moja), mada za mtaani, zakiutamaduni, afya, itikadi, dini, Qur’ani zinazo endana na akili za watoto wa kiislamu, zinazo onyesha kua kila kinacho andaliwa ni kwa ajili ya watoto, idhaa hii ilizinduliwa katika mwezi wa Rabiul Awwal mwaka (1432h), inarusha vipindi vyake kila siku ya Ijumaa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: