Hatua ya kwanza ya uwekaji wa marumaru za kifahari katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kupita zaidi ya nusu karne tangu zilipo wekwa

Maoni katika picha
Baada ya kufika katika uwekaji wa marumaru kwenye eneo linalo tenganisha sehemu ya juu na sehemu ya Kashi karbalai iliyowekwa katika ukumbi wenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi imeingia sehemu ya pili ya mradi huu, nayo ni sehemu ya kuweka marumaru katika sakafu yake, hivi karibuni kazi imeanza hatua ya kwanza, itafanywa kwa awamu awamu, chini ya utaratibu uliopangwa na kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwanamna ambayo wataweza kukamilisha ndani ya muda uliopangwa, na kwa kufuata uwiyano na kazi zinazo endelea sehemu zingine za jengo hili tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, amesema kua: “Baada ya kumaliza kuweka marumaru sehemu kubwa ya jengo la haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tulielekea katika ukumbi wake mtukufu na tumeanza hatua ya kwanza ya uwekaji wa marumaru za kifahari”.

Akaongeza kua: “Kazi hii imegawanywa katika hatua kadhaa, kila hatua inasehemu zake, kabwa ya ugawaji wa sehemu hizo tulifanya upembuzi yakinifu wa mradi wote na tukaweka mikakati, marumaru hizo zina nakshi na mapambo yanayo endana na yale yaliyopo sehemu zingine za Ataba ili kua na muonekano mzuri”.

Akabainisha kua: “Hatua ya kwanza ambayo inafanana katika utekelezaji na hatua zingine, inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Kuondoa marumaru za zamani.
  • - Kuondoa sehemu ya zege ya zamani na kurepea sehemu zilizo athirika.
  • - Kuziba sehemu zilizo pasuka kwa kutumia vifaa maalum.
  • - Kuweka zege ya awali ambayo juu yake itawekwa zege maalum yenye uwezo mzuri wa kushika marumaru na hairuhusu unyevunyevu itakayo kaa juu yake marumaru.
  • - Kutengeneza tabaka la chuma litakalokua chini ya zege.
  • - Kutengeneza mtandao wa maji, mawasiliano, zima moto na tahadhari na kuunganisha na sehemu ya uwanja wa haram tukufu kisha kuunganisha na mtandao mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kuanza kazi ya uwekaji wa marumaru kwa kufuata vipimo vilivyo pasishwa.

Kuhusu wasifu wa marumaru amesema kua: “Marumaru ni za kawaida na nadra (Malt onkos), zinaupekee wa aina yake, ni zakawaida, zenye rangi ya kawaida, zinauwezo mkubwa wa kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa, zina muonekano mzuri, nina ujazo wa sentimita (4) takriban”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa, dalili zinaonyesha kua haya ni mafanikio makubwa yanayo ongeza idadi ya kazi nzuri zilizo fanywa na mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: