Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein leo (7 Rabiul Aakhar 1440h) sawa na (14 Desemba 2018m) chini ya Uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amezungumzia vipengele vingi vya kimaadili vinavyo endana na mazingira halisi tunayo ishi, vipengele muhimu alivyo sema ni:

 • - Kuna baadhi ya watu huzidanganya nafsi zao.
 • - Kuna watu ambao hufanya mabaya zaidi kushinda mema na wanaweza kuwa katika nafasi za umma au binafsi.
 • - Kunatofauti kati ya mtu anayetafuta Dunia kwa mambo ya kidunia na anayetafuta kwa kujionyesha.
 • - Maana ya “Llabsu” ni pale mtu anaposema: Jambo hili limenichanganya sijui haki wala batili.
 • - Kuna baadhi ya watu huchanganikiwa na mambo kutokana na udhaifu wa akili zao hushindwa kutofautisha baina ya haki na batili.
 • - Baadhi ya watu huchanganywa na mambo yenye utata mkubwa na kuwafanya washindwe kupambanua.
 • - Baadhi huchanganikiwa pale ambapo mambo hayajawekwa wazi mbele yao.
 • - Baadhi huchanganikiwa kutokana na ushawishi wa watu fulani.
 • - Mwanaadamu anaweza kuchanganikiwa hapo anatakiwa awe na tahadhari na aulize.
 • - Wakati mwingine mtu hutaka asitoke katika mazingira ya kuchanganikiwa kwa sababu ndio chaguo lake, anataka awe juu ya kichuguu daima ili aweze kuomba samahani kwa makossa yake.
 • - Mwanaadamu anatakiwa awe makini, mwelewa na afanye mambo kwa hekima, asijifanye hajui kwa makusudi.
 • - Kuna ambao huzungumza jambo kwa kutilia shaka ili ajifanye kachanganikiwa na hajui uhakika.
 • - Mwanaadamu hujifanya hajui kwa makusudi ilia pate sababu ya kuomba samahani.
 • - Baadhi ya wakati mtu hujifanya hajui kwa makusudi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: