Idara ya usafi inafanya kazi kubwa ya kuweka mazingira safi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo jirani

Maoni katika picha
Idara ya usafi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa idara muhimu, kwani inanafasi kubwa sana ya kuweka muonekano mzuri katika mji mtukufu wa Karbala na ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayo zunguka haram, watumishi wa idara hiyo hutekeleza majumumu yao kwa ustadi mkubwa.

Mtandao wa Alkafeel umezungumza na kiongozi wa idara hiyo Ustadhi Riyaadh Khadhiir Muhsin ambaye amesema kua: “Watumishi wa idara yetu wanamajukumu mengi, wanajukumu la kusafisha sehemu zote za ukumbi wa haram tukufu, kuanzia milango, kuta na kila mahala ndani ya haramu tukufu, pamoja na kwenye sardabu na maeneo yote yaliyo ongezwa katika haram ndani na nje, pamoja na maeneo yote yanayo zunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na eneo la katikati ya haram mbili tukufu, bila kusahau sehemu za kuswalia na kupumzika mazuwaru watukufu”.

Akaongeza kua: “Kazi za idara hii hazijaishia kufanya usafi peke yake, wanafanya kazi zingine pia kama vile kusafisha vyoo vya Ataba tukufu, kufunga miamvuli nje ya haram tukufu na kutandika mazulia katika sehemu za kuswalia na katika sardabu, vilevile hupiga deki mara kwa mara ndani ya haram tukufu na katika barabara zinazo elekea kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunafanya kazi muda wote, watumishi wetu wanazamu tatu, wanatumia vifaa maalumu vya kufanyia usafi bamoja na mitambo mbalimbali, na wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu huongezewa wafanyakazi wa kujitolea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: