Kituo cha Rasuul A’adham cha Qur’ani chashiriki kwenye mradi wa Arshu Tilaawah kwa kuhudhuria kikao chake cha kila wiki

Maoni katika picha
Katika mfululizo wa vikao vya usomaji wa Qur’ani vya mradi wa Arshu Tilaawah, ambao ni miongoni mwa miradi inayo endeshwa na kituo cha kuandaa wasomaji ambacho kipo chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya, vikao hivyo hufanywa jioni ya kila siku ya Ijumaa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ugeni kutoka kituo cha Rasuul A’adham umekuja kushiriki katika kikao cha usomaji wa Qur’ani wiki hii.

Wasomaji wa Qur’ani wamesoma kwa mahadhi mazuri na sauti murua zilizo burudisha masikio ya wahudhuriaji na kufurahisha nyoyo zao, hakika kilikua kisomo kilicho hudhuriwa na watu wengi, mazingira yake yaliendana na utukufu wa haram hii, na kuunganisha utukufu wa Qur’ani na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa waliosoma ni: bwana Mauhubu Ahmadi Raadhi kutoka umoja wa wasomaji wa Qur’ani wa mtaa wa Salam na mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, na bwana Muhammad Zaliif mmoja wa wasomaji wa kwenye semina za Qur’ani, na bwana Munqidhu Idaani kutoka katika kituo cha Rasuul A’adham cha Qur’ani.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya inaendesha miradi mingi ya usomaji wa Qur’ani tukufu, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilaawah, unao lenga kunufaika na uwezo pamoja na vipaji vya vijana wa Iraq katika usomaji wa Qur’ani na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na kuviendeleza vipaji hivyo chini ya utaratibu maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: