Idara ya kubeba mazuwaru ni mfano bora katika kuwahudumia mazuwaru

Maoni katika picha
Zinafanyika juhudi za aina mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa watu wanaokuja kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), utawaona watumishi wanashindana kutoa huduma na kila mmoja kwa nafasi yake, miongoni mwa idara ambazo hufanya kazi mfululizo ni idara ya kubeba mazuwaru ambayo iko chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na vituo vya ukaguzi vya nje ambavyo vipo karibu na haram mbili tukufu, wanabeba mazuwaru kwa kutumia magari ya umeme.

Kiongozi wa idara ya utumishi na kubeba mazuwaru Ustadh Yasini Haashim Jaasim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunafanya kazi mfululizo ya kubeba watu wenye ulemavu na wazee na kuhakikisha hawapati usumbufu wowote, tumejipanga vizuri na tunatoa huduma kwa kutumia gari nyingi, kazi huongezeka zaidi kwenye msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, tunamiliki gari za aina tatu, tuna gari zinazo ingia watu (13) na zinazo ingia watu (7) na watu (5) zinafanya kazi muda wote.

Akaongeza kua: “Likitokea tatizo au msongamano wa watu kuna gari maalumu tunazo tumia, pamoja na gari tunazo tumia kila siku pia tuna gari za wagonjwa, ambazo hutumika rasmi pale zaairu anapopata tatizo au maradhi, pia tuna gari zingine ambazo hutumika kama gari za wagonjwa, hali kadhalika tunapo ombwa na vitengo vingine kupeba wageni wao hua tunafanya hivyo, tumeteua mahala maalumu kwa ajili ya kuchaji gari hizo ambapo ni karibu na kituo cha gari hizo, kila gari hutiwa chaja kwa muda maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: