Kawaida ya waumini shida zao nyingi huomba dua ili wasaidiwe na humtegemea Mwenyezi Mumungu mtukufu, hakuna kitu kikubwa zaidi ya kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutarajia akukidhie haja zako kwa utukufu wa mawalii wake na viumbe wake bora, nao ni Mtume Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s), umbali na ugumu wa mazingira vinaweza kua kikwazo kwa waumini wengi kushindwa kuja kuzuru malalo matukufu na kufanya ibada ya ziara na kuomba dua ndani ya haramu hizo ili wakidhiwe haja zao na kuondoshewa matatizo yao.
Idara ya Intanet ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ndani yake kuna mtandao wa kimataifa Alkafeel inawapa fursa waumini ya kutuma barua zao katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kupitia dirisha (ukurasa) wa barua kwa kaburi.
Huo ni ukurasa maalumu kwa ajili ya kufikisha barua na shida za waumini pamoja na kila jambo analofikiria katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), barua huzo huchapishwa kwa siri na kuwekwa ndani ya dirisha tukufu, kazi hiyo inafanyika kila siku tena kwa umakini mkubwa, watumishi wa kazi hiyo huhakikisha wanafikisha barua zote zilizo tumwa na watu ambao hawajabahatika kuja kumzuru mnyweshaji wenye kiu Karbala na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wake, tunapokea maelfu ya barua kila wiki kutoka nchi mbalimbali, pamoja na barua za waumini wanaoishi nje ya Iraq.
Ukurasa huu ni miongoni mwa kurasa zingine zilizopo katika mtandao, mtu yeyote anapoingia katika mtandao wa Alkafeel anaweza kuingia katika ukurasa huo pia, na anaweza kutuma barua kwa lugha yeyote miongoni mwa lugha zinazo tumiwa na mtandao, sio lazima utumie kiarabu, na barua hizo zitachapishwa na kuwekwa katika dirisha la kaburi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa maelezo zaidi unaweza kuangalia kupitia anuani hii: https://alkafeel.net/message/.