Mjumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Husseiniyya tukufu: Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud ni fahari kwa kila mwiraq

Maoni katika picha
Mjumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Husseiniyya bwana Fadhili Auz amesema kua shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, “Ni miongoni mwa miradi tunayo jifaharishia wairaq, kutokana na mafanikio waliyo pata, bidhaa zake zimekua kimbilio la wakulima wengi pamoja na watumiaji mbalimbali hapa Iraq, na limeweza kutoa ushindani katika soko kwa mashirika makubwa, na limekua ni ushindi mkubwa wa kiviwanda”.

Ameyasema hayo alipo tembelea shirika hilo na kuangalia bidhaa mbalimbali zinazo tengenezwa, ikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo, tiba na visafishio, alifuatana na mkuu wa idara ya utendaji Muhandisi Maitham Bahadeli ambaye alitoa maelezo kuhusu bidhaa wanazo zalisha.

Auz alifurahishwa sana na maendelea makubwa aliyo yaona katika shirika hilo, akasema: “Sio siri kwa mtu yeyote hakika shirika hili linatengeneza bidhaa bora kabisa, kwa hakika bidhaa za shirika hili ni fahari kwa waifaq wote”.

Akabainisha kua: “Shirika la Aljuud limetengeneza bidhaa bora za tiba, haya ni matokeo ya uzowefu na utaalamu wa watumishi wake, na wanaendelea kuboreka daima, shirika hili lilianza kidogo kidogo, limejiendeleza na kufikia hapa lilipo, sasa linamaendeleo makubwa katika kutengeneza bidhaa mbalimbali, nawapongeza sana watumishi wa shirika hili pamoja na viongozi wao, nashukuru juhudi zao ambazo ni fahari kwa wairaq wote”.

Kumbuka kua shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud limekua tegemeo kubwa katika sekta ya kilimo na viwanda hapa Iraq na hakika ni lakupigiwa mfano, kutokana na ubora wa hali ya juu wa bidhaa linazo tengeneza tena kwa njia za kisasa zaidi, na linatengeneza bidhaa nyingi zinazo husu viwanda na kilimo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu bidhaa zinazo tengenezwa na shirika hili unanaweza kupiga simu namba (07801035422) au (07801930125) au fika katika ofisi zake zilizopo Karbala barabara ya (Karbala / Najafu) mkabala na nguzo namba (1145).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: