Kutoka Basra: Mradi wa (Mimbari za nuru) wanachanganya kati ya kisomo na bayani maarufu kiimani

Maoni katika picha
Mradi wa (Mimbari za nuru) unao simamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani cha Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, unaendelea kufanya mahafali na vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani na nje ya mkoa wa Karbala, katika Ataba, mazaru, husseiniyyaat na misikiti, kwa ushiriki wa wasomaji wa Qur’ani kutoka ndani na nje ya Iraq chini ya utaratibu maalumu, mara hii kikao chake kimefanyika mkoa wa Basra katika wilaya ya Basra kwa mahadhi ya tilawa na bayani.

Mahafali imehudhuriwa na watu wengi, na ilihutubiwa na Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Aadil Alawiy aliye kua miongoni mwa wahudhuriaji wa hafla hiyo, akafuatilia kwa karibu usomaji wa wasomi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya ya Abbasiyya, Sayyid Hussein Halo na Mauhubu Hassanaini Aljazaairiy mmoja wa wanafunzi wa kituo cha Zaharaa pia ni mwanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, katika hafla hiyo pia rais wa umoja wa wadau wa Qur’ani katika mji wa Basra Shekh Abdulbasit Sahalani alizungumza na kutoa shukrani kubwa kwa Maahadi ya Qur’ani tukufu.

Kumbuka kua mradi wa (Mimbari za nuru) unalenga kufanya mahafali za usomaji wa Qur’ani katika mikoa mbalimbali, ni moja kati ya miradi inayo fanywa kwa kushirikiana baina ya Maahadi ya Qur’ani na taasisi au vikundi vya Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: