Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na wajibu walionao kisheria, kimaadili na kiidara kimefungua dirisha (ukurasa) maalumu katika toghuti utakao tumika kujibu maswali ya kidini na kifiqhi na kila jambo linalohusiana na maisha ya mwanaadamu ya kila siku.
Mjumbe wa kamati inayo simamia mtandao huo Shekh Bassim Fad’am amesema kua: “Kutokana na jukumu letu la kufundisha misingi ya Dini kwa watu wote, kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefungua njia ya mawasiliano ya wazi saa zote yanayo simamiwa na idara ya toghuti ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ili kurahisisha mawasiliano kati ya waumini na kitengo cha Dini kwa ajili ya kujibu maswali”.
Akaongeza kua: “Ukurasa huu umetengenezwa kwa namna ambayo ni rahisi kuutumia, unaweza kuingia kupitia anuani hii: https://alkafeel.net/religious/index.php? Weka swali lako sehemu iliyo andikwa “add_quest” maswali yote yatakusanywa na kupelekwa kwa Massayyid na Mashekh kwa ajili ya kuyapatia majibu kisha aliye uliza swali atatumiwa jibu kupitia barua pepe yake”.
Kumbuka kua kitengo cha Dini ni miongoni mwa vitengo vya kwanza kuundwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya maelekezo ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, kitengo hiki kina heshima kubwa sana katika akili na nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait na waislamu kwa ujumla na nisehemu muhimu inayo pokea na kushughulikia mahitaji ya mazuwaru, sambamba na kujibu maswali mbalimbali yanayo elekezwa kwao.