Wagonjwa na watu wenye ulemavu wanamzuru vipi Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kila mtu anajua namna Atabatu Abbasiyya tukufu inavyo wajali watu wanaokuja kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakati wote imekua ikifanya kila iwezalo kwa ajili ya kuwarahisishia utendaji wa ibada katika kaburi la mnyweshaji wenye kiu Karbala (Saaqi Atwaasha Karbala), hilo ndio jambo muhimu linalo zingatiwa katika kila kitu, hadi katika ujenzi wa haram tukufu na upanuzi uliofanyika.

Kwa ajili ya kurahisisha uingiaji wa mazuwaru katika hara tukufu, milango ya haram imetengenezwa kwa namna ambayo inamrahisishia kila mtu kuingia na kutoka bila usumbufu wowote, hii ni kwa sababu hakuna ngazi milangoni na milango inaendana na barabara zinazo zunguka haram, pia kuna sehemu maalumu zimeandaliwa kwa ajili ya kutumiwa na wagonjwa, wazee na watu wenye ulemavu wanaotumia mikokoteni au viti vya mataili, kwa ajili ya kuwawezesha kufanya ziara bila usumbufu wowote.

Hivi karibuni umefunguliwa mlango rasmi unaotumiwa na wagonjwa, wazee na watu wenye ulemavu wanao bebwa katika mikokoteni au viti vya mataili, upo karibu na mlango wa Alqamiy –Furaat- utawawezesha kutembea kwa uhuru bila kuchanganyika na watembea kwa miguu na kuwaepusha na msongamano wakati wa kufanya ziara, watafika mbele ya kaburi tukufu bila tabu. Pamoja na yote hayo pia kuna watumishi maalumu ambao wamepewa jukumu la kusimama eneo hilo na kuwasaidia mazuwaru wagonjwa, wazee na wenye ulemavu kwa kusukuma mikokoteni au viti vyao na kuwaongoza katika kufanya ziara kama watakua hawana mtu wa kuwaongoza au wakihitaji msaada huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: