Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika sherehe za wahitimu wa chuo kikuu cha Furaat Ausat

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika sherehe za wahitimu wa chuo kikuu cha Furaat Ausat katika kipindi chake cha nne wanacho kiita (kipindi cha ushindi na maendeleo), kupitia ujumbe maalum wa kitengo cha mahusiano ulioshiriki katika hafla ya wahitimu iliyo fanyika ndani ya chuo hicho, hafla hiyo imehudhuriwa pia na waziri wa elimu ya juu na utafiti wa kielimu Dokta Nabiil A’arajiy pamoja na rais wa kitengo cha kusimamia ubora wa elimu na mkuu wa mkoa wa Najafu Sayyid Luay Yaasiri, na idadi kubwa ya wakuu wa vyuo na wawakilishi wa Ataba za Najafu na Karbala, pia kulikua na idadi kubwa ya wageni, walimu, wanafunzi na familia za wahitimu.

Rais wa ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Hashim Hashimiy amesema kua: “Hakika leo ni siku nzuri kushiriki katika sherehe za wahitimu wa chuo hiki, huu ni wakati ambao wanachuma matunda ya mti waliopanda na kuuhudumia kwa miaka minne, tunawaombea mafanikio mema katika ujenzi wa taifa hili kwani linawahitaji zaidi”.

Naye waziri wa elimu ya juu na utafiti wa kielimu Dokta Nabiil A’arajiy amesema kua: “Mizani ya maendeleo ya kielimu katika vyuo vikuu hupimwa na matokeo ya elimu, wakufunzi na idara za vyuo vikuu zina nafasi kubwa ya kuangalia ubora wa huduma za kielimu, na ndio kipimo kizuri cha uwezo wa wahitimu”, akasema: “Kuna umuhimu wa kufanya tafiti ubunifu wenye faida katika jamii na kutatua kero za wananchini” akasisitiza kua: “Tunatarajia kuona mambo hayo kwa wahitimu wetu”.

Rais wa chuo Dokta Abdulkadhim Jafari Yasiriy alitoa shukrani za dhati kwa wahudhuriaji, wageni kutoka Atabatu Abbasiyya na wengine wote, pia katika ujumbe wake ameelezea mafanikio makubwa waliyo pata, ikiwa ni pamoja na kuanzisha vitengo vya masomo vinavyo saidia kutatua changamoto za jamii, sambamba na kufanya tafiti za kielimu na kuendesha makongamano ya kimataifa pamoja na kuchapisha majarida yanaho zungumzia fani mbalimbali za kielimu na ubunifu.

Katika hafla hii mashahidi wa Hashdi Sha’abi wametunukiwa vyeti vya heshima, na wanafunzi waliofaulu wakapewa zawadi baada ya maonyesho yaliyo fanywa na wanafunzi wakishirikiana na walimu wao pamoja na wajumbe wa ofisi ya utawala wa chuo, wakitanguliwa na waandishi wa habari wakiwa wameshika picha za mashahidi wa Hashdi Sha’abi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: