Makamo rais wa umoja wa maktaba za kiarabu: Sikutarajia kuona maendeleo niliyo yaona katika maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Makamo rais wa umoja wa maktaba za kiarabu Dokta Sefu Jaabiriy ameshangazwa sana na alicho kiona katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, amesema kua: “Sikutarajia kuona kiwango kikubwa cha maendeleo yaliyopo katika maktaba hii, jambo la kufurahisha zaidi, maktaba hii inamaendeleo makubwa katika mambo tofauti ndani ya miaka kumi tu, haya ni matokeo ya juhudi kubwa zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia watumishi wake”.

Ameyasema hayo katika ziara aliyo fanya asubuhi ya Jumanne (10 Rabiul Aakhar 1440h) sawa na (18 Desemba 2018m), ambapo aliangalia vitendea kazi na hazina kubwa iliyopo katika maktaba hiyo, pamoja na utendaji wa vitengo vyake na akapata ufafanuzi kutoka kwa watumishi.

Akaongeza kua: “Hakika vitendea kazi na vitengo vya maktaba hii ni fahari kwetu, hususan kituo cha kurepea nakala kale ambacho kinafanya kazi kubwa, wanaonyesha wazi namna wanavyo jali turathi za kiislamu”. Akaendelea kusema: “Kilicho nifurahisha zaidi ni mabadiliko ya kutumia namba katika nakala kale, ambayo ni fani ya kisasa inayo endana na maendeleo ya dunia katika kufanya utafiti, vifaa vinavyo tumika kurepea nakala kale ni vya kisasa zaidi, vifaa kama hivi niliviona katika chuo kikuu cha Kembriji nchini Uingereza, hii ni wazi kua maktaba ya Atabatu Abbasiyya inaubora wa kimataifa”.

Akasema: “Maktaba imepangiliwa vizuri mno, miongoni mwa mambo yaliyo nifurahisha pia ni namna wanavyo tengeneza makava, namna hii nimeiona kwa mara ya kwanza katika maktaba, japokua nimetembelea maktaba nyingi sana na vyuo vikuu mbalimbali vya Uingereza na Ujerumani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: