Kikosi cha wapiganiji cha Abbasi (a.s) chatangaza kukamilisha mishahara ya wapiganaji wake

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) umetangaza kukamilika kwa mishahara wa wapiganaji wake pamoja na viongozi wao baada ya juhudi kubwa zilizo fanywa na idara ya mali ya Hashdi Sha’abi, kikasisitiza kua kimekamilisha maandalizi ya lazima kwa ajili ya kuwapa mishahara wapiganaji wake wote pamoja na wale wa hakiba.

Uongozi umesisitiza umuhimu wa kuwapa kipaombele zaidi wale walioshiriki katika mapigano, na sio wapiganaji wapya, wakasema kua watafuatilia uteuzi mpya na orodha ya majina, kipaombele zaidi ni wapiganaji walioshiriki vitani na kuhudumia taifa.

Kikosi kimekanusha kua kinakusudia kusajili mpiganaji yeyote aliye jiunga baada ya vita.

Fahamu kua kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) ni moja ya vikosi vilivyo kua vinadai mishahara ya wapiganaji wake chini ya kanuni za idara ya mali, wapiganaji wake wamepewa jukumu la kulinda amani ya Hashdi na kufanya ukaguzi wakati wa ziara kupitia vikosi vyake kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuhakikisha mazuwaru wanafanya ibada kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: