Chuo kikuu cha Al-Ameed chafanya nadwa yenye anuani isemayo: (Nafasi ya maktaba za udaktari hapa Iraq katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu 2030m)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumatano (11 Rabiu Thani 1440h) sawa na (19 Desemba 2018m) kimefanya nadwa maalum kuhusu maktaba za udaktari hapa Iraq chini ya anuani isemayo: (Nafasi ya maktaba za udaktari hapa Iraq katika kufikia malengo ya maendeleo enelevu 2030m), nadwa hiyo imefanyika ndani ya ukumbi mkuu wa chuo na kuhudhuriwa na viongozi na wasomi kutoka ndani na nje ya Iraq.

Nadwa imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaibwa wimbo wa taifa pamoja na wimbo wa Atabatu Abbasiyya uitwao (Lahnul Ibaa), kisha akaongea rais wa chuo Dokta Jaasim Marzuki ambaye alisema kua: “Utamaduni wa Iraq ni mkongwe na miongoni mwa tamaduni za mwanzo kabisa katika historia ya mwanaadamu, wairaq ndio walio wafundisha watu ujenzi na umaridadi wakati ambao watu wengine walikua wanaishi katika mapango, wairaq ndio watu wa kwanza waliofundisha watu kuandika na shule ya kwanza duniani ilikua Iraq na maktaba ya kwanza ilikua Iraq, lengo la kuanzishwa kwa maktaba hiyo lilikua ni kusajili vitu vya jumba la ibada, na kuandika mafanikio ya kijeshi na ujenzi, iliitwa Sumariyya (Idiba) kwa maana ya “Jumba la usajili na utunzaji”.

Akaendelea kusema: “Kulikua na maktaba ya Aashuur Baanibaal (627 k.m) ya mwanzo kabisa yenye utaratibu bora duniani, ilikua maktaba ya kwanza kuwa ubora Duniani wakati huo, ilikua na vitu laki mbili na elfu hamsini, iikua na utaratibu wa kuazima na kurudisha vitabu pamoja na utaratibu wa kulipa faini kwa atakaye zidisha siku za kurudisha, kabati zake ziliwekwa alama za utambulisho kama inavyo fanyika zama hizi”.

Akaendelea kusema: “Baada ya hapo ndio zikafahamika tamaduni za kiarabu na kiislamu, kipindi hicho maktaba zilikua hazitambui utamaduni mwingine, likawa sawa na taa la elimu, na likaanza kutoa taasisi na wanachuoni mbalimbali, imeingizwa katika maktaba za umma kama vile maktaba ya Qurtwaba iliyoanzishwa na kiongozi Mustanswar bun Abdurahmaan Naasir mwaka wa (961m), na maktaba ya swahaba Abdullahi bun Abbasi na ibun Ameed, na maktaba ya kisekula iliyokua imefungamana na shule kama vile maktaba ya Darul-Hikmah, na maktaba za nyumba za ibada ambazo zilifungamanishwa na vyuo pamoja na misikiti kama chuo cha Qirawani”.

Kuhusu maktaba za vyuo Marzuki amesema kua: “Maktaba za vyuo ni sawa na taasisi zingine ambazo hufanya kila wawezalo kwa ajili ya kikidhi mahitaji ya wanufaika wake katika fani zao, maktaba za vyuo vya udaktari ni tofauti na maktaba zingine, miaka ya hivi karibuni maktaba hizi zinajitahidi kunufaika na teknolojia za kisasa, kuanzia mambo ya kompyuta na program zake na kuhakikisha wanafikisha elimu inayo hitajika kwa haraka kupitia maktaba za kielektronik na mitandao ya mawasiliano, pamoja na kutengeneza mitandao na kanuni za maktba ya udaktari ya kitaifa”.

Akasisitiza kua: “Maktaba za vyuo vya udaktari leo hii zinahitajika kutumia elimu za kisasa na kutumia vifaa vya kisasa, kwa ajili ya kuboresha huduma zake na kukidhi mahitaji ya watumiaji, maktaba zinatakiwa kua na vitu vipya na mnufaika anatakiwa awe na weledi wa kutumia maktaba hizo”.

Kisha akazungumza rais wa umoja wa maktba za kiarabu Dokta Sefu bun Abdullahi Aljaabiriy.

Katika nadwa hiyo pia jumla ya mada tatu ziliwasilishwa, mada ya kwanza iliwasilishwa na Ustadh Wasiim Twalib Mahdi kutoka kituo cha machapisho ya kielimu (makao makuu) / chuo kikuu cha Al-ameed, yenye anuani isemayo: (Viashiria vya kupima ubora wa huduma za maktaba), mada ya pili ikawasilishwa na Ustadh Hassanaini Mussawiy kutoka kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat ambacho kipo chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu isemayo: (Maendeleo endelevu katika maktaba za udaktari za Iraq), na mada ya tatu ikawasilishwa na Dokta Ikram Juburiy kutoka chuo kikuu cha Bagdad – kitivo cha udaktari, isemayo: (Kujisajili na kupata machapicho ya kielektronik yenye elimu bora zaidi bure).

Kisha Dokta Ikram Juburiy akarudi tena kusoma maazimio ya maktaba za udaktari za Iraq, nadwa ikafungwa kwa kugawa zawadi za vidani kwa washiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: