Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chatangaza mradi wa kiutafiti uitwao (Sisi na maswala ya mwanamke) na chatoa wito kwa wasomi washiriki kufanya utafiti

Maoni katika picha
Katika mwendelezo wa miradi ya kiutafiti inayo lenga kutatua changamoto za jamii, kituo cha kiislamu na masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa wito kwa watafiti na wasomi, washiriki kufanya utafiti katika mradi uliopewa jina la (Sisi na maswala ya mwanawake) nao ni mradi wa utafiti wa vikundi unao lenga kuibua maswala ya wanawake katika jamii ya kiislamu, na matokea yake katika kipindi cha karne mbili kutokana na khutuba za kiislamu zinazo husu maswala ya wanawake, pamoja na kutazama miradi mingine ya kimagharibi au iliyo dhihiri hivi karibuni katika ulimwengu wa kiislamu ulioathirika na umagharibi.

Kituo kimeteua mada za kufanyiwa utafiti ambazo ni:

  • 1- Uislamu na mwanamke: (misingi ya uislamu katika maswala ya mwanamke).
  • - Mwanamke katika Qur’ani.
  • - Mwanamke katika hadithi tukufu.
  • - Nidhamu za haki za mwanamke: (Haki na wajibu, ushiriki katika siasa na jamii, ukarimu, familia na mengineyo).
  • - Kulinganisha baina ya mwanamke katika uislamu na katika Dini zingine.
  • - Kulinganisha baina ya mwanamke katika uislamu na katika nchi za magharibi.
  • - Shubha zilizopo: (Urithi, fidia, umama, uongozi, ndoa za matala, kukeketwa, ndoa za utotoni, hijabu, talaka na mengineyo).
  • - Kasoro za uchumba wa kimila kwa wanawake (watu na sheria).
  • 2- Unyanyasaji wa kijinsia: (maelezo na madhara).
  • - Historia na harakati za Moroko.
  • - Historia na harakati za ulimwengu wa kiislamu na kiarabu.
  • - Sheria na utekelezaji: (harakati za wanawake, tabia za wanawake, lugha za wanawake, mtazamo na uwelewa wa wanawake, siasa za wanawake, saikolojia za wanawake, fani za wanawake, tarbiya ba taalim na mambo mengine pamoja na maswala ya jinsia).
  • - Kasoro za khutuba za kimagharibi upande wa wanawake.
  • 3- Maazimio ya umoja wa mataifa na njama za walimwengu kuhusu mwanamke (mtazamo na madhara).
  • - Misingi ya utangazaji na kanuni za kazi.

Tafiti za mada zilizo tajwa zitumwe katika ofisi ya wahariri kupitia barua pepe ifuatayo: islamic.css.lb@gmail.com . kwa kufuata utaratibu ufuatao:

  • - Wasiliana na ofisi ya wahariri kwa ajili ya kutaja mada uliyo chagua.
  • - Tanguliza muhtasari wa utafiti kabla ya kuanza kuandika utafiti mzima.
  • - Kutotosheka na kuandika ukamilifu pekeyake unatakiwa kuandika na mapungufu.
  • - Utafiti usizidi kurasa (25).
  • - Tafiti zitumwe ndani ya muda wa miezi (5).
  • - Utafiti utakua ni miliki ya kituo na kitakua na haki ya kuusambaza na kuufasiri.
  • - Mtafiti atapewa zawadi ya pesa.
  • - Kuyafanyia kazi mapendekezo ya kamati ya wataalamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: