Waziri wa kilimo atembelea mashamba ya Atabatu Abbasiyya tukufu na asema: Miradi yake inalenga kuendeleza sekta ya kilimo hapa Iraq

Maoni katika picha
Katika ziara yake ya kwanza mkoani Karbala tangu ateuliwe kua waziri wa kilimo, Dokta Swaaleh Hussein Alhusseiniy amesisitiza kua: “Miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya inastahiki pongezi, kwani inamchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo hapa Iraq na kulirudisha taifa katika nafasi yake ya kujitegemea”.

Ameyasema hayo katika ziara aliyo fanya pamoja na ujumbe ulio fatana naye asubuhi ya Alkhamisi (12 Rabiul Aakhar 1440h) sawa na (20 Desemba 2018m), ambapo ametembelea baadhi ya miradi ya kilimo ya Atabatu Abbasiyya kama vile mradi wa vitalu vya Alkafeel na mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, katika ziara hiyo aliongozana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar aliye kua akimpa maelezo na ufafanuzi kuhusu miradi wanayo fanya vitendea kazi wanavyo tumia na mafanikio waliyo pata.

Alhusseiniy akasema kua: “Sisi kama wizara tunaunga mkono miradi hii, na tunatoa wito kwa sekta husika waje wajifunze kwenu na wanufaike kutokana na uzowefu wenu, kwani miradi hii inasaidia kupunguza uagizaji wa chakula kutoka nje na kutegemea chakula cha ndani”.

Akabainisha kua: “Tunawapongeza watendaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu na tunawaomba waendelee kufanya miradi hii yenye faida kubwa na matokeo ya moja kwa moja ya matumizi ya raia wa Iraq, pia inasaidia kupunguza tatizo la ajira sambamba na kutumia zana za kisasa zinazo endana na maendeleo ya Dunia katika sekta ya kilimo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: