Haya ndio yaliyo maazimio ya kituo cha Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat katika siku ya lugha ya kiarabu

Maoni katika picha
Hafla ambayo hufanywa kila mwaka ya siku ya lugha ya kiarabu na kusimamiwa na kituo cha Al-Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni, ambayo imefanyika asubuhi ya leo (13 Rabiul Aakhar 1440h) sawa na (21 Desemba 2018m), kuna maazimio kadhaa yamefikiwa katika hafla hiyo, ambayo yamewasilishwa na Dokta Aadil Nadhiir kama ifuatavyo:

  • 1- Kutunga kanuni za kulinda lugha ya kiarabu katika vyuo vikuu na ndani ya jamii.
  • 2- Kubadilisha selibasi za kufundishia lugha ya kiarabu ili iendane na maendeleo ya elimu katika ufundishaji wa lugha, kwa kuingiza program mpya katika shule za msingi na sekondari (upili).
  • 3- Kuwataka walimu wa vyuo wafundishe masomo yote kwa lugha fasaha ya kiarabu na waandike vitabu vya fani mbalimbali kwa lugha ya kiarabu.
  • 4- Luninga (tv) zitumie lugha fasaha ya kiarabu katika taarifa za habari na mambo mengine.
  • 5- Mitandao ya mawasiliano itumie lugha fasaha ya kiarabu ili kushajihisha zaidi matumizi ya kiarabu fasaha (fus-ha).
  • 6- Tunaomba hafla za siku ya lugha ya kiarabu zifanywe kwa wingi na taasisi za umma na binafsi ili kuonyesha umuhimu wa lugha ya kiarabu na kuilinda.
  • 7- Kuongea na waziri wa Tarbiyya ili kuwe na masomo yatakayo saidia kukuza lugha ya kiarabu na matumizi ya kiarabu fasaha kwa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: