Marjaa Dini mkuu abainisha mambo yanayo takiwa kuzingatiwa ili kuweza kutanguliza maslahi ya umma dhidi ya maslahi binafsi.

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya leo (13 Rabiul Aakhar 1440h) sawa na (21 Desemba 2018m) iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, Marjaa Dini mkuu amebainisha mambo yanayo takiwa kuzingatiwa ili kuweza kutanguliza maslahi ya umma dhidi ya maslahi binafsi, akasema kua tunahitaji kunzingatia mambo kadhaa:

Kwanza: kuzingatia mfumo wa kifikra –nafafanua maana ya neno hilo- ni wazi kua maumbile ya ubinafsi ndiyo humfanya mtu ajali maslahi binafsi na kupuuza maslahi ya umma, kinyume chake lazima kuwe na misingi ya kimaadili inayo elekeza hisia hizo katika njia sahihi katika mambo ya umma na mambo binafsi, bila kusahau tunamsukumo wa kimaadili pia, lazima tuangalie misingi ya maadili ambayo ni muhimu katika malezi ya mwanaadamu kuanzia katika ngazi ya familia, shule, chuo na taasisi zingine, yatupasa tuzingatie mfumo wa fikra na idikadi, wakati wote tunatakiwa kumkumbusha mwanadamu kua watu wengine wana utu sawa na wewe, wanatamani kupata manufaa kama wewe, hata kama watatofautiana na wewe dini, tabaka au madhehebu fahamu kua ni ndugu zako katika ubinaadamu au dini, jambo hili lazima lijengwe katika fikra zetu na tulifanyie kazi.

Pili: mfumo wa kimaadili (akhlaq) ambao hubainisha umuhimu wa manufaa na maslahi ya wengine na kukidhi mahitaji yao, mfumo wa kujitolea na kusaidia watu pamoja na kuwatakia mambo mazuri, inatakiwa kuelezea faida na manufaa ya mfumo huu.

Tatu: kuandaa mazingira mazuri, tunakusudia nini tunaposema mazingira mazuri? Kuwa kigezo, mtu mwenye madaraka, aliyepewa madaraka na watu anatakuwa kuwa kiigizo chema kwa wengine, mwalimu ni kiigizo chema kwa wanafunzi, na mhadhiri wa chuo kikuu ni kiigizo chema kwa watu wengine, daktari, mhandisi, mwajiriwa kila mmoja anatakiwa awe kiigizo chema kwa wengine, mazingira mazuri humjenga mtu kuhudumia watu wengine.

Nukta ya nne na muhimu; taasisi za kutunga sheria na za kiutendaji zilinde maslahi ya umma, wakati mwingine malezi pekeyake hayatoshi, watu wengi wanatuambia zungumzeni kadha na kadha katika khutuba za Ijumaa, ndio sisi tunazungumza lakini mawaidha na nasaha hunufaisha baadhi ya nyakati, kama kusipokua na kanuni na sheria zinazolinda maslahi ya umma na kuhudumia umma pamoja na kuzuia mtu yeyote asitangulize maslahi binafsi na kuwadhuru wengine hayatakua na faida, inatakiwa kuwe na sheria zinazo linda mali za umma na kusimamia utendaji, zinazo simamia haki na kulinda uvunjifu wa haki, kama hakuna mambo hayo hatutaona matunda ya mawaidha na nasaha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: