Elimu ya Dini na maelekezo yanamnufaisha vipi zaairu wa Atabatu Abbasiyya tukufu?

Maoni katika picha
Screen zimesambaa katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika baadhi ya milango ya haram hiyo, pamoja na screen kubwa iliyopo katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, zina nafasi kubwa ya kufukisha fikra na kutoa elimu anayo hitajia zaairu, hususan elimu ya dini yenye mchango mkubwa wa kumuongoza zaairu, elimu hiyo inatolewa kwa njia za kisasa.

Kitengo cha Dini ndio kinacho husika na kutoa elimu hiyo kupitia idara ya tabligh, huandaa ratiba ya mwezi mzima inayo husisha hadithi maneno ya hekima na mambo ya kitamaduni, pamoja na kuelezea matukio ya dini yaliyopo katika mwezi huo na mambo mengine, baada ya kuandaliwa hutumwa katika idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya, nayo ni idara ya mafundi wanaohusika na kuweka taarifa hizo katika screen za matangazo, na huandaa vipande vifupi vya video vinavyo endana na taarifa zinazo kusudiwa kutangazwa, kazi hiyo husimamiwa na watu waliobobea katika fani hiyo.

Screen hizo pia huonyesha ratiba za mambo ya dini na utamaduni yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kurusha dua, ziara na mambo mengine, yanamuwezesha zaairu kusoma moja kwa moja katika screen hizo wakati wa kufanya kwake ziara katika sehemu hiyo tukufu.

Fahamu kua lengo la mradi wa Screen za matangazo ni kunufaika na teknolojia ya kisasa, sambamba na kunufaika na huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru watukufu, pia screen hizo hutumika kurusha matangazo ya moja kwa moja katika ziara makhsusi, mahafali na shughuli mbalimbali zinazo fanywa na Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: