Kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) kinatoa mafunzo kwa watumishi wake kuhusu namna ya kukabiliana na moto na namna ya kutumia vifaa vya kuzimia moto, kwa ajili ya kujiweka tayali kupambana na tatizo lolote linalo weza kutokea –Allah atuepushie- chini ya jopo la wakufunzi kutoka kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Mkufunzi wa semina hii Dokta Bilali Jabbaar Jaasim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Semina hii ni moja ya semina nyingi tunazo endesha, katika semina hii tumefundisha mambo mengi, kubwa zaidi ni namna ya kukabiliana na moto unao anza pamoja na vitu vinavyo weza kushika moto, kulikua na mfano wa kuwasha moto na kuonyesha namna ya kuuzima, pamoja na njia mbadala zinazo weza kutumika katika kuzima moto”.
Akaongeza kua: “Wamefundishwa mbinu nyingi za kuzima moto mkubwa na mdogo, pamoja na hatua muhimu zinazo takiwa kufatwa wakati wa kuzima moto, mwisho wa semina walifanya mazowezi makali ya kuzima moto yaliyo onyesha uwezo mkubwa walio nao wa kuzima moto na kuweka mazingira salama nyumbani na kazini”.